muhtasari

Latest Article Get our latest posts by subscribing this site

SAUZI YARINDIMA MSIBA WA NELISON MANDELA...


Wanajeshi wakiwa wameubeba mwili wa hayati Mandela kuelekea ofisi za serikali jijini Pretoria.
Mwandishi Wetu na Mitandao
MAOMBOLEZO ya kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini, Nelson Mandela yanaendelea, kubwa kuliko ni nchi hiyo yenye kilomita za mraba 2,798 kufurika waombolezaji kutoka pande zote za
dunia na hivyo, hakuna pa kukanyaga na hali hii ni mwanzo na mwisho!
Nelson Mandela.
Habari kutoka jijini Johannesburg nchini humo zinasema, msiba wa Mandela umebadilisha ghafla hali ya maisha ya raia wa nchi hiyo.
HOTELI HAZINA NAFASI
Hoteli nyingi, hasa katika Miji ya Pretoria na Johannesburg (alikofia Mandela), nyumba za kulala wageni, hoteli na sehemu nyingine zenye kuhifadhi watu zimejaa baada ya wateja kukodi kwa muda wote wa msiba hadi mazishi.
Wageni wanaoingia nchini humo kwa ratiba zao za kabla ya kifo wamekuwa wakipata tabu sehemu za kulala, wengine kugeuza wanakotoka.
Familia ya marehemu Mandela ikifuatilia ibada ya kumbukumbu.
Baadhi ya wenyeji waishio nchini humo wamewasiliana na ndugu zao wanaotaka kwenda, kusitisha safari ili kupisha shughuli za mazishi yatakayofanyika Desemba 15, mwaka huu.
BIDHAA BEI JUU
Licha ya kwamba kipato cha kawaida kwa wananchi wake ni cha chini, bei ya bidhaa, hasa vyakula imepanda na wafanyabiashara wengi wanaitumia fursa hiyo kujineemesha.
Rais wa Marekani, Barrack Obama akiwapungia maelfu ya wananchi waliohudhuria ibada ya kumkumbuka Mandela katika Uwanja wa FNB, Soweto, Afrika Kusini.
MIPAKA HAIPITIKI KAMA ZAMANI
Tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya kifo cha Mandela ambapo wengi waliweza kuingia nchini humo bila kubanwa na ukaguzi wa kina, kwa sasa ulinzi umeimarishwa ambapo kila muingiaji anaulizwa maswali mengi, hasa yanayohusu usalama.
MAGAIDI WATUPIWA MACHO ZAIDI
Usalama nchini humo tangu kutokea kwa kifo cha Mandela umekuwa ukiwatupia macho zaidi magaidi wa kimataifa ambao wanaweza kutumia mwanya wa maombolezo kupenya na kusababisha maafa.
Baadhi ya waombolezaji.
GRACA MACHEL, WINNIE MANDELA HAKUNA BIFU
Juzi ndani ya Uwanja wa FNB uliopo Mtaa wa Soccer City nchini humo wakati wa zoezi la kumuaga marehemu Mandela, kivutio kikubwa kilikuwa kwa wanawake wawili waliowahi kuwa na uhusiano na kiongozi huyo.
Winnie Medekizela Mandela, aliyewahi kuwa mke wa Mandela mpaka kutoka kifungoni na Graca Machel aliyekuwa mke mpaka kifo cha Mandela, walitazamwa na waombolezaji wengi kufuatia historia zao kutokuwa na migongano.
Wawili hao, mara kadhaa wamewahi kupiga picha ya pamoja na mzee huyo wakiwa na nyuso za furaha huku wote wakiwa wamemkumbatia.
Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Jakaya Kikwete (wa nne mstari wa pili kulia kutoka juu) na mkewe Mama Salma wakifuatilia ibada ya kumbukumbu ya Nelson Mandela.
OBAMA AHUTUBIA NDANI YA JUKWAA LENYE VIOO VYA KUKINGA RISASI
Akitoa hotuba yake kwa wananchi wa Sauzi na waombolezaji wengine duniani kote, Rais wa Marekani, Barack Obama alionekana ndani ya jukwaa lenye vioo visivyoweza kupitwa na risasi (bullet proof).
DUNIA YAANDIKA HISTORIA MPYA
Kuwepo kwa Rais wa Marekani, Barack Obama na Rais wa China, Xi-Jinping kunasemekana ni kuandikwa kwa historia mpya ya dunia kwani viongozi hao hawajawahi kukutana nje ya nchi zao.
Kingine kilichoonekana ni kuandikwa kwa historia mpya ya dunia ni tukio hilo kuwa la kwanza kukutanisha viongozi wazito wa duniani kwa wakati mmoja.
Inadaiwa hata wanaokwenda kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa hawakufikia uzito wa kwenye msiba wa Mandela.
Marais mbalimbali wakiambatana na ujumbe mzito kutoka katika nchi zao walihudhuria msiba huo, ukiachana na watu wengine maarufu na viongozi wa kawaida.
JINA LA KIKWETE LAWA LA KWANZA KWENYE ORODHA
Katika hali iliyoonesha mshikamano kati ya Afrika Kusini na Tanzania, jina la Rais Jakaya Kikwete lilikuwa la kwanza katika orodha ya marais waliokuwa kwenye mwaliko.
Jambo hilo limeongeza hamasa na uhusika wa moja kwa moja kwa Watanzania juu ya msiba huo kutokana na umoja, ushirikiano na kuaminiana kulikooneshwa na Sauzi.
Juzi, Jumatatu, Desemba 9, mwaka huu katika sherehe za Miaka 52 ya Uhuru, zilizofanyika kitaifa, Uwanja wa Uhuru, Dar, Rais Kikwete alizungumzia namna marehemu Mandela alivyoipenda Tanzania na uhusiano mwema wa nchi hizi mbili.
Hilo lilijidhihirisha baada ya Sauzi kumweka Rais Kikwete wa kwanza, akiwaongoza marais na viongozi wengine waliohudhuria msiba na shughuli za mazishi ya shujaa huyo.
NAMBA 3 YAWAMALIZA VIGOGO NCHINI HUMO
Pamoja na yote, namba 3 imeonekana kuweka historia ya kipekee nchini humo kwa kuhusika na vifo vya viongozi wake wakuu.
Mpigania haki mwingine mkongwe, Oliver Tambo aliyezaliwa Oktoba 27, 1917 naye alifariki mwaka 1993 (Aprili 24). Walter Sisulu, alikuwa mpigania uhuru sambamba na Tambo na Mandela, naye alifariki dunia mwaka 2003 (Mei 5, alizaliwa Mei 18, 1912).
Kifo cha Mandela kilichotokea Desemba 5, 2013 kinazidi kutia shaka katika orodha ya namba 3 kila baada ya miaka 10.
Marehemu Nelson Mandela ambaye zoezi la kuuaga mwili wake linakamilika leo kwenye uwanja huo, atazikwa Jumapili ijayo. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi 
- Amina.

RAIS KIKWETE AWASILI SOUTH TAYARI KUHUTHURIA MAZISHI YA RAIS NELSON MANDELA...


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Afrika Kusini usiku wa kuamkia leo  Desemba 10, 2013 tayari kuhudhuria maziko ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
 
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali, Ibada Kuu ya kumwombea Marehemu itafanyika leo Desemba 10, 2013 katika Uwanja wa FNB Johannesburg, ambapo viongozi na watu mashuhuri mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wataungana na wananchi wa Afrika Kusini katika shughuli hiyo ya kihistoria. 
 
Kesho Disemba 11 hadi Disemba 13, 2013 mwili wa marehemu utakuwepo katika jengo la Union Building ambapo viongozi na watu mashuhuri watatoa heshima zao za mwisho. Jengo hilo ni kama Ikulu ya nchi hiyo.
 
Maziko yatafanyika Desemba 15, 2013 katika kijiji cha Qunu, Mthatha, Easter Cape
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Rais Kikwete akisalimiana na Mwambata wa Kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania Afrika kusini katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake mwenye ushungi kichwani ni Mama Salma Kikwete
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahman Kinana.
 PICHA NA IKULU

JE JOSEPH KONY ATAJISALIMISHA?...

Kony, ni kiongozi wa kundi la waasi la LRA, na anatakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa madai ya uhalifu wa kivita.
Marekani ilikuwa imeahidi kumtuza dola milioni 3.3 yeyote mwenye taarifa itakayopelekea kukamatwa kwa Kony
Hii ni mara ya kwanza kwa miaka mingi, kwa taarifa kuhusu aliko Kony kutolewa.
Pia mnamo siku ya Jumatano, mjumbe maalum wa muungano wa Afrika kuhusu LRA, Francisco Madeira, aliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa, kuwa aliona ripoti kuwa Kony anaugua ugonjwa mbaya sana usiojulikana.
Mnamo mwezi Aprili, jeshi la Uganda lilisitisha msako dhidi ya Kony katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, likisema kuwa linabiliwa na mashambulizi makali kutoka kwa serikali waasi walipochukua mamlaka baada ya mapinduzi.
Joseph Kony pamoja na wapiganaji wake walio kati ya 200-500, wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya Uganda kwa zaidi ya miaka 20.

HATARI...RAIA WA KIGENI ANASWA NA MAFUVU...

Polisi nchini Burundi wanasema zaidi ya mafuvu 40 ya binadam yamepatikana katika makao ya raia mmoja wa Italia anayefanya kazi nchini humo.
Giussepe Favaro alikamatwa mwezi uliopita baada ya mafuvu mawili yaliyonuiwa kusafirishwa kwa ndege kunaswa katika uwanja wa ndege nchini Burundi.
Kwa mujibu wa polisi mafuvu hayo yalinuiwa kusafirishwa hadi nchini Thailand.
Polisi hata hivyo hawajatoa taarifa zaidi na mwandishi wa BBC nchini Burundi anasema watu wana shauku ya kutaka kujua mafuvu hayo yalitoka wapi na yalikua yatumike kivipi.
Kumekuwepo ripoti za sehemu za miili ya binadam kutumika katika ushirikina hasa katika nchi jirani ya Tanzania,lakini haifahamiki kwanini mafuvu yaliyopatikana hapo awali yalikua yakipelekwa Thailand.
Bw Favaro amekua akiishi nchini Burundi kwa miaka kadhaa.
-bbc

RAIS KIKWETE NA KENYATA WA KENYA WAKUTANA AFRIKA KUSINI KUZUNGUMZA JAMBO MUHIMU....NI JAMBO GANI PATA HABARI...

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliyemtembelea na kumsabahi hotelini kwake Sandton Sun jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini, leo Oktoba 5, 2013 (picha: Ikulu ya Tanzania)
Picture
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliyemtembelea na kumsabahi hotelini kwake Sandton Sun jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini, leo Oktoba 5, 2013
Picture

MAGAIDI (AL-SHABAAB)WAIZINDUA TANZANIA USINGIZINI...




TUKIO la kigaidi lililotokea nchini Kenya katika jengo la biashara la Westgate, limeizindua Tanzania na hivyo wamiliki wa majengo makubwa ya biashara likiwemo Mlimani City jijini Dar es Saalam kuimarsha ulinzi.
Tangu kutokea kwa tukio hilo linalodaiwa kutekelezwa na kundi la kigaidi la Al-Shabaab la nchini Somalia na kusababisha vifo vya watu 67 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, nchi za Afrika Mashariki zimeanza kuchukua tahadhari kubwa katika kukabiliana na vitendo hivyo.
Tanzania Daima Jumapili jana lilishuhudia msafara mkubwa wa magari uliokuwa ukiingia katika jengo lenye maduka mbalimbali ya biashara la Mlimani City yakifanyiwa upekuzi wa kina, huku madereva wakitakiwa kuteremka na kuyaacha tupu.
Aidha, baadhi ya wafanyakazi wa jengo hilo waliovalia vifaa maalumu walikuwa wakivipitisha chini ya magari yaliyoingia katika jengo hilo kwa umakini wa hali ya juu tofauti na siku za nyuma ambazo watu waliingia na kutoka bila kukaguliwa.
Mmoja wa kiongozi wa ukaguzi huo ambaye ni raia wa kigeni, alionekana kuwa makini na kuwataka wateja wote walioingia na magari yao ndani ya eneo hilo kuyaweka pembeni ili yafanyiwe upekuzi.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa madereva, Juliaus Janco alisema kuwa ni vyema utaratibu huo ukawekwa katika kila jengo lenye msongamano wa watu ili kukabiliana na maafa yanayoweza kutokea, hasa katika kipindi hiki cha uwepo wa magaidi.
Alisema kuwa pamoja na baadhi kuonekana kukerwa na utaratibu huo, lakini wanapaswa kuelewa kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza hofu iliyojengeka sasa, hasa watu wanapoingia katika majengo kama hayo.
Katika hotuba yake ya juzi, Rais Jakaya Kikwete pia aligusia tukio hilo la kigaidi la Kenya akisema kuwa anafahamu kuwa baada ya tukio hilo watu wengi nchini wameingiwa na hofu kuhusu usalama.
“Ni hofu ya msingi kwani Agosti 8, 1998, Ubalozi wa Marekani hapa nchini ulishambuliwa na magaidi na ndugu zetu 11 wasio na hatia walipoteza maisha,” alisema.
Alisema kuwa tangu shambulio la mwaka 1998, serikali imekuwa inajenga uwezo wa vyombo vya ulinzi na usalama kupambana na ugaidi katika nyanja mbalimbali.
“Tunaendelea kujiimarisha bila kusita siku hadi siku. JWTZ, Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa wamekuwa na ushirikiano wa karibu kwa ajili hiyo. Juhudi zetu hizo ndizo zinazotufanya tuwe salama hadi sasa,” alisema.
Rais aliongeza kuwa baada ya tukio la Kenya, vyombo vya ulinzi na usalama vimeimarisha mikakati yao maradufu. Kwamba pamoja na kujizatiti hawawezi kusema kuwa tukio la kigaidi halitaweza kutokea nchini.
“Uhakika huo hatuna kwani hata mataifa makubwa na tajiri yameshambuliwa. Kilicho muhimu ni kuendelea kuchukua tahadhari na wananchi kusaidia ili vyombo vyetu vifanikiwe zaidi.
“Hali kadhalika, tumewataka watu wote wenye shughuli zinazokusanya watu wengi kama vile maduka, maofisi, mahoteli, migahawa waweke kamera za ulinzi nje na ndani ya maeneo yao,” alisema.
Pia aliwataka waangalie uwezekano wa kuweka vifaa vya upekuzi (metal detectors and x-rays). Kwamba anajua watu wanaweza kulalamikia usumbufu au gharama, lakini gharama na hasara ya kushambuliwa ni kubwa zaidi kuliko ya usumbufu huo.
Kenya yataja watuhumiwa ugaidi
Wakati huohuo, habari kutoka Nairobi, Kenya zinasema kuwa nchi hiyo imetoa majina ya watu wanne ambao inasemekana walifanya shambulio dhidi ya jengo la maduka la Westgate wiki mbili zilizopita.
Watu ambao wote ni wanaume, walionekana kwenye picha za kamera za usalama zilizopatikana Westgate baada ya jengo hilo kushikiliwa na Al-Shabaab kwa siku nne.
Msemaji wa jeshi aliwataja watu hao kuwa ni Abu Baara al-Sudani, Omar Nabhan, Khattab al-Kene na Umayr.
Taarifa zinasema kuwa wawili kati yao wana uhusiano na al-Qaeda na mmoja ana uhusiano na wapiganai wa al-Shabaab ambao walikiri kuhusika na shambulio la Westgate.
-tanzania daima

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger