muhtasari

Latest Article Get our latest posts by subscribing this site

HATARI…MAUAJI YAITIKISA NCHI...JAMBAZI LAENDESHA MAUAJI YA WATU 8 KWA SIKU TATU MFULULIZO, IGP MANGU ASHTUSHWA, APELEKA WAPELELEZI KUMSAKA…

Mauaji ya kutisha yametikisha wilaya ya Tarime kiasi cha kumfanya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, kutuma timu maalum kutoka makao makuu ya jeshi hilo inayohusisha kamisheni ya Operesheni kufanya uchunguzi.

Hatua ya kupelekwa kwa timu hiyo inatokana na mauaji ya mfululizo katika mji wa Tarime ambayo ipo kwenye himaya ya Kanda Maalum ya Polisi ya Tarime na Rorya ambayo yametokea kwa watu wanane katika kipindi cha siku tatu.

Mauaji hayo yanadaiwa kufanywa na jambazi mwenye silaha katika mji wa Tarime mkoani Mara kwa siku tatu kuanzia Jumatatu hadi jana.

Mmoja wa watu waliouawa ni askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Koplo Zakaria Chacha Mwita ambaye ni mtoto wa marehemu Meja Jenerali Mwita Marwa.

Pia wamo aliyekuwa Mhandisi Ujenzi Wilaya ya Rorya, aliyetajwa kwa jina la David Mwasi Misiwa.

Wengine ni mfanyabiashara, Samuel Richard Mohenga na huku Jeshi la Polisi likisema kuwa linaendesha msako.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Royra, Justus Kamugisha, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema kuwa mtu anayesadikiwa kuwa jambazi akiwa na bunduki kwa siku tatu kuanzia Januari 26, mwaka huu usiku aliua watu saba kwa kuwapiga risasi  na kujeruhi kadhaa.

Aliwataja wengine kuwa ni mwendesha bodaboda, mkazi wa kijiji cha Nkende, Juma  Marwa Nyaitara, Erick Lucas Makanya, mfanyabiashara  wa bucha mkazi wa kijiji cha Rebu, Juma Mwita Mroni na mkazi wa kijiji cha Kenyamanyori, Robert Chacha Kisiri.

Jana asubuhi, wakazi wa mji wa Tarime na vitongoji vyake walimfananisha mtu aliyekuwa amevaa koti refu na mtuhumiwa wa mauaji hayo na kutaka kumshushia kipigo, lakini aliokolewa na polisi waliorusha risasi hewani na kumpeleka katika kituo cha polisi.

Kamanda Kamugisha aliwashauri wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mara watakapomuona mtuhumiwa.

 Alisema polisi wanafanya msako katika vijiji vya Kenyamanyori, Rebu, Nkende, Mogabiri na Kibumaye katika kata za Kitare, Turwa na Binagi kwenye Tarafa ya Inchage.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele wakishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tarime jana  walitembelea maeneo ya vijiji ambavyo wakazi wake wameuawa na jambazi hilo.

TIMU YA MAKAO MAKUU
Alizungumzia timu iliyotumwa Tarime, Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Paul Chagonja, alisema kuwa ni ya wapelelezi na Intelijensia na inakwenda kuongeza nguvu katika juhudi zinazofanywa na mkoa wa Mara kuhakikisha jambazi huyo anakamatwa ili kuondoa hofu kwa wananchi.

Chagonja alisema juhudi za kumsaka jambazi huyo zinaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi.

SOPHIA SIMBA ALAANI MAUAJI
Wakati huo huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba,  amelaani maauji ya wanawake watano waliotaarifiwa kuuawa katika wilaya za Musoma, Butiama na Rorya mkoani Mara.

Alisema wizara inasisitiza kuwa mtazamo huo ni hasi na unakwenda kinyume cha haki za binadamu hivyo jamii haina budi kuachana na imani zinazosababisha mauaji.
 
“Wizara inahimiza wananchi kupinga dhana potofu zinazopelekea mauaji ya wanawake ikiwa ni pamoja na imani za kishirikina, uchu wa kupata utajiri wa haraka, kulipiza kisasi na kuendeleza hulka ya ukatili katika jamii,” alisema.

Alisema: “Mauaji dhidi ya wanawake yanapotokea katika jamii zetu yanarudisha nyuma juhudi za serikali katika kuzuia ukatili dhidi ya wanawake katika jamii kutokana tu na tofauti za kimaumbile.
 
Wizara inaitaka jamii itambue kuwa wanawake wana haki ya kuthaminiwa utu wao na kushiriki haki zote za msingi bila ubaguzi wowote ambao unaweza kuhatarisha haki yao ya kuishi ambayo ndiyo haki kuu kuliko haki zote,” alisema na kuongeza:

“Kushamiri kwa mauaji ya kikatili wanayofanyiwa wanawake katika wilaya za mkoa wa Mara ni jambo ambalo linasababisha hofu kubwa miongoni mwa wanawake. Mauaji hayo yanawakosesha amani na utulivu na hivyo kuzorotesha ari yao katika shughuli za uzalishaji mali.”

CHANZO: NIPASHE

KATIBA MPYA KUTUMIKA KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO...KATIBA YA TANGANYIKA YAPENDEKEZWA IPEWE MAANDALIZI YA MIAKA MINNE...

Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya, imeelekeza kipindi cha mpito ambacho pamoja na mambo mengine, kitaandaa mazingira ya Katiba hiyo kutumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. 
 
“Kufanya maandalizi na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kuzingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014 na kufanya maandalizi ya mambo yote muhimu kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014,” inasema sehemu ya rasimu hiyo.
 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia imependekeza kipindi cha mpito cha miaka minne kuanzia tarehe ya kuanza kutumika kwa Katiba Mpya ili sheria zilizopo ziweze kubadilishwa.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alisema jana kwamba katika kipindi hicho cha mpito utakuwa ni muda wa kutungwa kwa Katiba ya Tanganyika. 

Warioba alisema pia katika kipindi hicho, utakuwa ni muda wa mgawanyo wa rasilimali baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za nchi washirika.
 
“Katika kipindi hicho pia utakuwa ni muda wa kufanya maandalizi na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kuzingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 2014,” alisema.
 
Warioba alisema katika kipindi hicho, Katiba ya Zanzibar itafanyiwa marekebisho ili kuwiana na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014.
 
Sehemu ya Rasimu ya Katiba ya Muungano, imependekeza kuwa maoni yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, yanaweza kutumika kutengeneza Katiba ya Tanganyika.

>>Mwananchi

HII BALAA...SHANGAZI WATOTO WAFUNGIWA NDANI KWA MIEZI SITA NA SHANGAZI...

“TUNAJUA shangazi anatutesa kwa sababu baba na mama wapo mbali, kama wangekuwepo hapa tusingeteswa hivi. Tunamuomba baba, tunamuomba mama kama watasoma habari hii waje watuchukue turudi nyumbani, shangazi anatutesa sana, wala hatukutegemea,” ndivyo alivyoanza kusema mtoto Hassan Yusuf (5) ambaye ni mkubwa kwa wenzake, Hussein Yusuf (5) na Rehema Said (5). 
 
Ikifika mahali mtoto mdogo anasema anawakumbuka wazazi wake kwa sababu ya mateso anayoyapata ugenini ujue ni zaidi ya ukatili, tena ni ukatili wa kutisha.
 
Watoto hao, kwa sasa wanaishi Nzasa ‘A’, Kata ya Charambe, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam na ndiko walikopatia mateso yote.

MAMBO YALIPOANZA KUTIBUKA
Wiki iliyopita, watoto hao waliokolewa na majirani katika kifungo cha miezi sita ndani huku afya zao zikiwa zimedhoofu kwa kukosa chakula.

Ilidaiwa kwamba, watoto hao Hassan na Hussein ambao ni mapacha na Rehema,  walifungiwa katika banda la shangazi yao aitwaye Asia Bora ambalo ujenzi wake haujakamilika. Wamekuwa wakiishi humo kwa kula mabaki ya vyakula jalalani.

USHUHUDA WA MAJIRANI
Wakizungumza na gazeti  la Uwazi  hivi karibuni, majirani wa nyumba hiyo walimweleza mwandishi kuwa watoto hao wamekuwa wakionekana  nje ya nyumba hiyo mara chache sana wakiwa wanagombania mabaki ya vyakula kwenye jalala.

“Tumekuwa tukiwaona nje mara chache kwenye jalala. Unajua, Asia (shangazi yao) aliwachukua kwa kaka yake, Kijiji cha Namakongoro Kata ya Lihimalyao huko Kilwa mkoani Lindi.
 
“Tukasikia lengo lake aje kuishi nao kwa vile yeye Mungu hamkujalia kupata watoto. Lakini maisha hapo kwake yakawa siyo mazuri kwa kipato kwa mama huyo.
 Mmoja wa majirani hao aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Ramadhan yeye alikwenda mbele zaidi kwa kusema:
 
“Hapo awali tulikuwa tukiwaona wakitoka nje na kucheza na watoto wetu huku wakiwa na afya nzuri. Asia akatueleza kuwa ni watoto wa nduguye, amewachukua huko kijijini.

“Baada ya muda fulani tukawa hatuwaoni, tulidhani amawarudisha kwao, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinakwenda mbele tukawa tunawaona mara chache wakiwa jalalani wanapigania mabaki ya chakula.
 
“Kuna siku mimi niliwakamata wakiwa wamebeba mfuko wa rambo wenye kinyesi, walikuwa wanakuja kutupa katika maeneo yetu, nikawarudisha nao kwa shangazi yao. Kumbe nyumba wanayoishi haina choo ndiyo maana wamekuwa wakijisaidia kwenye rambo.

“Siku moja walipotoka nje kutafuta chakula jalalani, mimi na majirani wenzangu tuliwauliza wanaishije? Wakatuambia hawapewi chakula na shangazi yao akitoka asubuhi harudi mapema, akirudi inakuwa ni usiku sana wao wakiwa wameshalala.

“Inasikitisha sana kuwaona watoto hawa wanaachwa peke yao kutwa nzima bila mtu wa kukaa nao na wamekuwa wakifungiwa ndani kwa muda mrefu sasa, ila huwa wanakiuka masharti na kutoka kwa ajili ya kutafuta mabaki ya chakula.

Jirani huyo akaendelea kuanika mateso ya watoto hao: “Kwa kuwaonea huruma tumekuwa tukilazimika kuwapa chakula, lakini Asia anaporudi na kugundua hilo anawapiga, kwa hiyo wakawa waoga kuja kuchukua chakula. Mimi niliumia hadi machozi.”

Jirani: “Baadaye wakawa hawaonekani, lakini cha ajabu mara nyingi tukiamka asubuhi tunakuta mifuko ya rambo yenye vinyesi imetapakaa, tukimweleza Asia inakuwa ugomvi.
 
“Siku moja baada ya shangazi yao kuondoka, nilikwenda kuwachungulia ndani, nikawaona wamekonda sana, wamepauka na wamevaa nguo zilizochakaa.

“Nilitokwa machozi, nililazimika kuwaita wenzangu nao walipofika hakuna aliyejizuia kulia. Tukasema hawa watoto watakufa, ndiyo tukaamua kuwaokoa kwa kupeleka taarifa kwa mzee Dadi Salum ambaye ni polisi jamii wa hapa.

POLISI JAMII NAYE ALIA
“Mzee Dadi naye alipofika na kuwaona kwa macho alilia, watu wakaanza kukusanyika, tukawatoa nje watoto, kila mmoja aliwaonea huruma. Tuliwachukua hadi Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Nzasa A.

SHANGAZI MTU ANUSURUKA KIPIGO
“Hatujui ni nani aliyempigia simu Asia, kwani muda mfupi tu tukasikia yupo nyumbani kwake. Uongozi wa mtaa ulimfuata, walipofika, wanawake wenzake hasa wale anaochukua nao mkopo wa fedha benki walitaka kumpiga wakimuuliza pesa anapeleka wapi.

“Hata hivyo aliokolewa na polisi jamii ambao walimchukua na kumweka katika Bajaj na kumpeleka Kituo cha Polisi Mbagala kwenye Dawati la Jinsia na Watoto, watoto nao pia walipelekwa huko.”

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nzasa A, Mrisho Salum alikiri kuwapokea watoto hao wakiwa katika hali mbaya kiafya, wakapelekwa polisi. Akawataka wananchi kutokaa kimya mara wanapoona vitendo kama hivyo.

Mwandishi alifika hadi kituo cha polisi na kuambiwa na askari mmoja kuwa mapacha walichukuliwa na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Othman Mbwana  aliyedai ni babu yao.

Mbwana alidai kwamba ameamua kuwachukua watoto hao wakaishi nyumbani kwake wakati akifanya mawasiliano na wazazi wao.
 
“Kwanza nitawapeleka hospitali wakatazamwe afya zao, ila nimesikitishwa sana na hali hii, sijajua ni kwa nini watoto hawa wamefikia hatua hii,” alisema Mbwana.

Rehema yeye alichukuliwa na mjomba wake aitwaye Sood Ismail ambaye alidai anakwenda kukaa naye hadi hapo atakapofanya mawasiliano na wazazi wa huyo mtoto, akisema kitendo cha Asia kimeidhalilisha familia.
 
RPC TEMEKE ATUPIA NENO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo amewataka wananchi kufichua vitendo viovu ndani ya jamii na amewapongeza vijana wake wa ulinzi shirikishi kuokoa maisha ya hao watoto.

Source: Gazeti  la  Uwazi/ Global publisher

RAIS KIKWETE AWASILI SOUTH TAYARI KUHUTHURIA MAZISHI YA RAIS NELSON MANDELA...

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Afrika Kusini usiku wa kuamkia leo  Desemba 10, 2013 tayari kuhudhuria maziko ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
 
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali, Ibada Kuu ya kumwombea Marehemu itafanyika leo Desemba 10, 2013 katika Uwanja wa FNB Johannesburg, ambapo viongozi na watu mashuhuri mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wataungana na wananchi wa Afrika Kusini katika shughuli hiyo ya kihistoria. 
 
Kesho Disemba 11 hadi Disemba 13, 2013 mwili wa marehemu utakuwepo katika jengo la Union Building ambapo viongozi na watu mashuhuri watatoa heshima zao za mwisho. Jengo hilo ni kama Ikulu ya nchi hiyo.
 
Maziko yatafanyika Desemba 15, 2013 katika kijiji cha Qunu, Mthatha, Easter Cape
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Rais Kikwete akisalimiana na Mwambata wa Kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania Afrika kusini katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake mwenye ushungi kichwani ni Mama Salma Kikwete
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahman Kinana.
 PICHA NA IKULU

TAARIFA YA SAMSON MWIGAMBA KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WARAKA WA MKAKATI WA MABADILIKO 2013 ...

TAARIFA YA SAMSON MWIGAMBA KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WARAKA WA MKAKATI WA MABADILIKO 2013

Jumatano, 27 Novemba 2013
Jana katika taarifa kwa waandishi wa habari, Mhe. Tundu Lissu na Mhe. John Mnyika waliudanganya umma kuhusu waraka unaohusu Mkakati wa Mabadiliko 2013. Katika maelezo yao waheshimiwa hawa, pamoja na mambo mengine, walidai kuwa waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni feki. Ukweli ni kwamba:

Ninathibitisha kwamba waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ni sahihi neno kwa neno kama nilivyousoma katika magazeti ya HabariLeo, Jamhuri na Rai, pamoja na nakala iliyopo Jamii Forum. 

Ili kuthibitisha kwamba waraka ule ndio wenyewe, nawatumieni ‘soft copy’ kutoka kwenye kompyuta mpakato (laptop) yangu ambako ndiko ulikoibwa na viongozi wa chama baada ya kunipora kwa nguvu laptop yangu Oktoba 25 na kukaa nayo hadi jioni ya Oktoba 28.
 
 Naomba kila mtu asome neno kwa neno waraka ninaowapa leo halafu afananishe na ule uliopo kwenye magazeti na kwenye mtandao ili mjiridhishe kama kweli sio wenyewe. Kama Lissu na wenzake wana mpango wa kuuchakachua waraka huu wamekwama!

Waraka huu si wa uhaini wala mapinduzi wala usaliti kama inavyodaiwa na akina Lissu. Huu ni waraka wa kusaka ushindi katika uchaguzi halali ndani ya chama ambao ulikuwa ufanyike Desemba 2013, na ambao sasa umesogezwa mbele. 
 
Napenda ijulikane kwamba wakati wa uchaguzi si jambo la ajabu kuwa kwa wanachama kuwaunga mkono wagombea tofauti. Nimekuwa karibu na Mwenyekiti Mbowe kwa miaka mingi na ninajua kwamba yeye naye anao mkakati tena unaohusisha mbinu haramu za kuhakikisha anammaliza Zitto na yeye kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi huo. Wanaoshiriki mkakati wake ni pamoja na Lema, Lissu na wakurugenzi kadhaa waliopo makao makuu.
 
Waraka huu ulipaswa kuwa siri ndani ya watu watatu tu (M1, M2 na M3) na haikutarajiwa kwamba ungevuja kwa jamii. 

Bahati mbaya viongozi wa chama baada ya kuunasa waraka huu kutoka kwenye komputa yangu mpakato (laptop), na baada ya kikao cha Kamati Kuu, waliamua, kwa jazba na bila kutumia busara ya kiuongozi, kuusambaza waraka huo kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuwakomoa na kuwadhalilisha waandaji. 

Sasa baaada ya kugundua madhara ya waraka huo machoni pa jamii wameamua kuukana. Ni ajabu kwamba wanaukana waraka ambao waliusambaza wenyewe. 
 
Nasisitiza kwamba mambo yaliyopo kwenye waraka ni bayana na dhahiri. Sibahatishi kwa sababu mimi nimefanya kazi makao makuu kama Mhasibu Mkuu hadi Mwezi Aprili 2012. 
 
Ni kwa kutambua uozo uliopo katika uongozi wa chama makao makuu niliona umuhimu wa kubadilisha uongozi kwa njia za kidemokrasia ili tukiokoe chama na hatukuwa na nia wala sababu za kuanika haya yote kwenye umma. 
 
 Kwa sababu za chuki na kukosa busara za kiuongozi huyo anayeitwa Mwanasheria Mkuu akawashauri viongozi wetu kijinga wauanike waraka mbele ya macho ya watanzania. 

Wangekuwa na akili na busara baada ya yote haya kutokea wangejiuzulu au kuitisha uchaguzi mara moja.

Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa siku nyingi sana na wametamani kumfukuza siku nyingi. 

Hata hivyo, ninawashauri watafute sababu nzuri za kumfukuza uongozi na hata uanachama kwa sababu yeye hahusiki na waraka wetu wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 hata chembe, pamoja na kwamba yeye ndiye alikuwa na bado ndiye mlengwa mkuu, kama atakubali.

Samson Mwigamba (M3)
Arusha

AIBU:- MWANAMKE APIGA PICHA ZA UTUPU BAADA YA KUZIDISHA POMBE

Mwanamke mmoja ambaye ni mke wa mtu na mkazi wa jiji la Mwanza amejikuta ndani ya aibu nzito baada ya kulewa pombe na kisha kujipiga za utupu...

Habari zinaarifu kuwa mwanamke huyo alitinga ndani ya gesti moja yenye kaunta ya baa mida ya mchana na kuanza kupata vinywaji 

Muda mfupi baadae, mzee mmoja alijumuika na mama huyo na kuendelea kutandika bia mpaka ilipopanda utosini.

Baada ya kulewa kupita kiasi, wawili hao walijisogeza ndani ya chumba kimoja cha gesti hiyo na kuanza kusaliti ndoa yake huku akijifotoa akiwa mtupu. Picha hizo zilinaswa na mumewe baadae kupitia simu yake.

Popular Post

Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger