
Mbali na Selemani, mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni raia ambaye anatambulika kwa jina la Hamis Mwanya (22), ambao walifikishwa jana mahakamani hapo mbele ya Hakimu Nyigulila Mwanseba.
Wakili wa Serikali, Mwanaisha Komba, alidai mbele ya Hakimu Mwanseba kuwa Julai 19, mwaka huu katika eneo la Tazara wiliyani Temeke, jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao walikutwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo manne pamoja na vipande 12 vya meno hayo vilivyo na thamani ya Sh. milioni 121.5, ambayo ni mali ya Serikali.
Hata hivyo, washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi isipokuwa Mahakama Kuu na pia upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.
Hakimu Mwanseba aliahirisha shauri hilo hadi Agosti 7, mwaka huu, na washitakiwa walirudihswa rumande.