muhtasari

Home » » USAJILI MANCHESTER UNITED - KWANINI INAWEZA IKAWA RAHISI KUMRUDISHA MODRIC EPL KULIKO CESC FABREGAS

USAJILI MANCHESTER UNITED - KWANINI INAWEZA IKAWA RAHISI KUMRUDISHA MODRIC EPL KULIKO CESC FABREGAS



Manchester United wanaweza kuhamishia nguvu kwa kiungo wa Real Madrid Luka Modric baada ya usajili wa kiungo wanayemtaka kwa udi na uvumba Cesc Fabregas kuonekana unaelekea kushindikana.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari barani ulaya United wanaandaa ofa ya kuanzia ya paunfi millioni 25 kwa ajili ya kumrudisha Luka Modric EPL katika harakati za David Moyes kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo. 
Modric amekuwa hana nafasi ya kudumu ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Madrid tangu alipohamia timu hiyo akitokea Tottenham mwaka 2012. Amekuwa akiivutia United kwa muda mrefu tangu alipokuwa akikipiga pale White Hart Lane.
Safu ya kiungo ya Madrid ina lundo la wachezaji - wakiwemo Xabi Alonso, Mesuti Ozil, Sami Khedira, Pepe, Modric mwenyewe na sasa wameongezwa wahispania ambao wametoka kusaidia timu yao ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 kubeba ubingwa wa Euro - Illaramendi na Isco. Hivyo uwepo wa kijiji hichi katikati ya dimba la Madrid unafanya nafasi ya kucheza kwa Modric kuwa ngumu.
Real Madrid kuuza wachezaji ili kuweza kufidia pengo la fedha ambazo wameshalipa kuwanunua Illaramendi na Isco - huku wakiwa wanatakiwa kutoa mzigo mkubwa kuweza kumnunua Gareth Bale. Kumuuza Modric kunaweza kuwa rahisi kama watapata ofa nzuri kutoka kwa Manchester United au klabu nyingine yoyote, kwanza kwa sababu wanahitaji fedha za usajili wa Bale na pili tayari wanao wachezaji wa kuziba pengo la Modric endapo ataondoka.

Luka Modric anatajwa kuwa na thamani ya €35millioni wakati Cesc Fabregas anatajwa kuwa thamani €45millioni - kwa fedha ambazo United wametoa ofa kwa klabu ya FC Barcelona mpaka sasa €35m zingekuwa na uwezo wa kumsajili Modric kabisa.

 
TAKWIMU
Luka Modric na Cesc Fabregas wote wana uzoefu wa ligi kuu ya England, aina a=yao ya mchezo haitofautiani sana japokuwa kuna baadhi ya vitu wanazidiana. Wote ni wazuri katika kupanga mashambulizi ya timu lakini wana udhaifu katika ukabaji. Wakati Modric ni mzuri wa mipira mirefu kama ilivyokuwa kwa Paul Scholes, Fabregas ni mzuri wa pasi fupi fupi na pasi za mwisho.

Katika driblling - Modric ni mzuri zaidi kuliko Fabregas. 
Cesc ana udhaifu wa kupiga mipira ya krosi - wakati eneo hilo linamudiwa vizuri na Modric, mchezo ambao Manchester United wanatumia sana. 
chanzo:shaffih dauda

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger