Shughuli katika uwanja wa
kimataifa wa ndege JKIA nchini Kenya, zinatarajiwa kurejea katika hali
ya kawaida kuanzia usiku wa manane.
Waziri wa usafiri, Michael Kamau, amesema kuwa
sehemu iliyotengewa marasia kuingilia na kutoka kwenye uwanja hyuio
itatumiwa na wageni kutoka nchi za kigeni watakaowasili katika uwanja
huo.Safari kadhaa za ndege za kimataifa zilirejea leo huku ndege za shirika la ndege la Kenya zikitua na kuruka katika hali inayoweza kusemekana kuwa ya kawaida.
Ndege za kimataifa zimeanza kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa jijini Nairobi JKIA, siku moja tu baada ya kitengo cha kuwasili wageni kuchomwa na moto mkubwa na kulazisha uwanja huo kufungwa kwa masaa kadhaa.
Ndege ya kwanza ya kimataifa kuwasili katika uwanja huo ni ile iliotoka Uingereza na baadaye nyengine kutoka Tanzania na Bangkok zikawasili.
Wachunguzi hata hivyo wanatathmini chanzo chake.
Wakati huo huo Rais wa Marekani, Barack Obama amesema ataisaidia serikali ya Kenya katika kukarabati uwanja huo wa ndege baada ya moto mkubwa kuuteketeza hapo jana.
Katika ujumbe wake wa simu, Obama alisisitiza kuwa Marekani iko tayari kuisadia Kenya katika hali ile yoyote kutokana na ushikiano wake na Kenya.
Obama pia aliwapa pole familia zilizowapoteza wapendwa wao katika mashambulizi ya bomu ya Agosti 1998 mjini Nairobi.
Manmo Jumatano, moto mkubwa uliotokea majira ya asubuhi, uliharibu kitengo cha kuwasilia wageni wa kimataifa.
Vikundi vya wachunguzi viliwasili katika uwanja huo kufanya uchunguzi wao kubaini kilichosababisha moto huo.
Abiria walikwama kutokana na mkasa huo ingawa waliweza kuondolewa nje ya uwanja kwa ajili ya usalama wao huku baadhi wakiangalia mizigo yao ikiteketea wasijue la kufanya. .
Rais Uhuru Kenyatta aliwasili katika uwanja huo na kujionea uharibifu uliotokea na kiisha kutoa taarifa yake kupitia kwa msemaji wake Esipisu aliyesema kuwa chanzo cha moto huo kinachunguzwa.
chanzo:BBC