
Mama mmoja awaomboleza baadhi wa watu waliouwawa na jeshi ,Misri
Tamko hilo la baraza la usalma linakuja siku moja tu baada ya watu wapatao 638 kuuwawa wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya waandamanaji wafuasi wa Muslim Bortherhood.
Waandamaji hao wamekuwa wakitaka Bwana Morsi aliyeondolewa uongozini arudishwe maradaraki.
Wakati huo huo rais wa Marekani Barack Obama ameshutumu hatua ya serikali ya muda ya Misri akisema haukuwa na sababu za kutosha.
"tunasikitishwa sana na unyama uliofanyiwa raia wa kawaida " , amesema Obama huku akitangaza kuwa zoezi la kijeshi la pamoja kati ya Marekani na Misri ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika mwezi ujao umefutwa.
Rais Obama amesema ushirikiano kati ya nchi hizo mbili hauwezi kuendelea wakati raia wanauwawa.

Rais Obama ashutumu serikali ya Misri
Wanachama hao 15 walishindwa kuafikiani kuhusu jinsi ya kukabiliana na hali ya Misri, huko jeshi likizidi kukaza kamba.
Kwa kawaida Urusi na China huwa zinapinga hatua yeyote ya baraza la usalama kuingilia maswala ya ndani ya nchi yeyote ile. Hivyo katika kikao hicho cha dharura , Urusi na China hazikibadili msimamo wao wa jadi , bado walipinga kuwa Misri na jeshi lisiingiliwe bali njia ya maridhiano itafutwe.
Pengine hii ni kutokana na swala la Chechnya ambalo bado linaisumbua Urusi huko China ikihangaishwa na tatizo la Tibet.
Taarifa zinasema China ilikataa katakata kutia saini taarifa rasmi ya baraza la usalama la kulishutumu jeshi la Misri kwa kusababisha umwagikaji wa damu na mauaji.
-BBC