Na Habel Chidawali na James Magai, Mwananchi
(email the author)
Posted Ijumaa,Agosti9 2013 saa 12:32 PM
Posted Ijumaa,Agosti9 2013 saa 12:32 PM
Kwa ufupi
- Awataka Watanzania kuwa na subira wakati huu ambapo bado hajakabidhiwa rasmi ofisi na kuahidi kuwa mtumishi wa watu wote pale atakapoanza rasmi majukumu aliyokabidhiwa.
Dodoma. Msajili mteule wa Vyama
vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amewataka Watanzania kutulia na
kusubiri utendaji wake atakapokabidhiwa rasmi jukumu hilo jipya
alilopewa na Rais Jakaya Kikwete.
Mutungi aliteuliwa kushika wadhifa wa msajili wa
vyama vya siasa kuchukua nafasi ya John Tendwa ambaye amestaafu. Tendwa
aliiongoza taasisi hiyo kwa miaka 13.
Mutungi alisema: “Ninafahamu nina majukumu mazito
mbele yangu, lakini siwezi kusema chochote kwa kuwa sijakabidhiwa rasmi
ofisi. Ninachotaka kusema ni kwamba nitakuwa mtumishi wa kila mmoja.”
Alikataa kusema kuwa akianza kuzungumza mambo
mengi kwa sasa wakati hajaingia rasmi kazini haitakuwa na maana yoyote
na badala yake ataonekana kuwa anawahisha mambo.
Jana katika Mahakama Kuu ya Dodoma, ilikuwa tabu
kumpata kiongozi huyo hali iliyoonyesha huenda alikuwa katika maandalizi
ya kuweka mafaili yake katika hali nzuri kabla ya kuwaaga watumishi
wenzake na kwenda kuanza majukumu mapya.
Wasaidizi wake wa karibu hawakuwa tayari kuelezea
alikuwa na kazi gani hasa, lakini walimwambia mwandishi kuwa Jaji
alikuwa na majukumu mengi kiasi cha kukosa nafasi ya kuzungumza na mtu.
Hata hivyo, alipompigia simu msajili huyo licha ya
kukataa kuzungumza mambo mengi kuhusu nafasi yake hiyo mpya, lakini
alionekana kuwa na ushirikiano wa kutosha na kuwataka wananchi wasubiri
kitambo ili akabidhiwe. Juzi akizungumza na gazeti hili, Tendwa alikataa
kumshauri Mutungi na kusema kuwa anaamini atafanya kazi kwa mujibu wa
sheria na taratibu kama ambavyo miongozo inavyotaka.
“Mutungi atafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kama ataanza kubezwa na wanasiasa afahamu kuwa sasa ndiyo anafanya kazi sawasawa.
Mawakili wamlilia
Mawakili mbalimbali wameelezea kuridhishwa na
uteuzi wa Jaji Mutungi kuwa msajili wa vyama vya siasa, huku
wakimmwagia sifa kuwa ni mtu sahihi katika wadhifa huo na kwamba ana
uwezo.
Wakizungumza na Mwananchi jana kwa nyakati
tofauti, mawakili hao walisema Jaji Mutungi anafaa katika nafasi hiyo
kulingana na sifa yake ya ujaji na uzoefu wa kisheria na kwamba wana
imani kuwa ataiongoza vyema ofisi hiyo.
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika
(Tanganyika Law Society- TLS), Francis Stolla na mawakili Richard
Rweyongeza na Jerome Msemwa, walimzungumzia Jaji Mutungi.
-MWANANCHI
-MWANANCHI