Rais wa mpito nchini Misri,
anasema kuwa juhudi za kimataifa kutuliza mgogoro wa kisiasa nchini humo
ambao ulitokana na kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Mohammed
Morsi, zimegongwa mwamba.
Adly Mansour na washirika wake walioko kwenye
jeshi, wamekuwa wakishauriana na wajumbe wa kimataifa kutoka Marekani,
Muungano wa Ulaya , Qatar na Milki za kiarabu.Zaidi ya watu 250 wameuawa kwenye mgogoro huo wa kisiasa tangu Morsi kuondolewa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai baada ya maandamano ya umma.
Maseneta wawili wa Marekani siku ya Jumanne waliitisha mazungumzo kati ya serikali ya mpito na vuguvugu la Muslim Brtherhood
Lakini serikali ya mpito hii leo ilitangaza kuwa mazungumzo ya kidiplomasia yamefika kikomo leo.
Iliongeza kusema kuwa juhudi hizo hazijafanikisha chochote.
Brotherhood walaumiwa
Serikali imesema kuwa inalaumu vuguvugu la Muslim Brotherhood kwa kutofanikiwa kwa juhudi za amani na matukio mengine yanayohusu utovu wa usalama na ukiukwaji wa sheria.Mjumbe wa Marekani Bernardino Leon na mwenzake naibu waziri wa mambo ya nje wamekuwa Misri kwa siku kadhaa kufanya mazungumzo ya kupatanisha pande hizi mbili katika mgogoro huu.
"tutajaribu kadri ya uwezo wetu kuhakikisha watu wanashauriana,'' alisema msemaji wa EU Michael Mann.
"ni Muhimu kuona kuwa kunakuwa na kipindi cha mpito chenye kuzingatia demokrasia...tutaendelea na juhudi zetu,'' aliongeza msemaji huyo.
Waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi amekuwa mjumbe wa hivi karibuni aliyetarajiwa kufanya mzungumzo na mwenzake wa Misri, waziri mkuu na rais wa mpito pamoja na maafisa wengine mnamo Jumatano