Kagame ni vigumu kuthamini ushauri wa JK kwa sababu zifuatazo:-

1) JK haifahamu vizuri historia ya Rwanda ambayo imejengwa kwa damu. Watutsi ambao ni wachache wametumia damu kuwatawala wahutu ambao ni wengi na jinsi ya kuwawezesha wengi (Wahutu) bila kuathiri haki za wachache (Watutsi) ndani ya Rwanda imeshindikana hadi leo.
Mfupa uliomshinda Mzee fisi je JK atauweza kwa utendaji huu tunaoufahamu hapa nchini?

a) JK kushauri mahasimu hao wakae meza moja bila ya kujua ajenda na mikakati ya kufanikisha vikao tajwa kwa Kagame anaona ni upuuzi ambao mjenga hoja -JK- lazima azabuliwe kofi ili aache kujiingiza kwenye mambo yasiyomhusu.

b) JK katika masuala ya Muungano na kero zake amekuwa akiendelea kutegemea kamati ya viongozi wa kitaifa watokanao na chama chake cha CCM tu bila ya kutafuta wapinzani katika kushauriana nao. Hivyo aidha ni unafiki au usahaulifu tu kumshauri Kagame afanya yale ambayo yeye mwenyewe JK hana mpango wa kuyafanya.
Charity always begin at home.................

c) JK katika uundaji wa kamati ya marekebisho ya katiba katumia ubabe wa uwingi wa wabunge wa CCM Bungeni katika kupitisha sheria ambayo imempa yeye madaraka ya kurekebisha Katiba atakavyoona inafaa na ushirikishwaji wa wananchi ni changa la macho tu. Sasa yawaje amshauri Kagame kujenga mazingira ya ushirikishwaji wa mahasimu wake jambo ambalo yeye mwenyewe JK hayuko tayari kulifanya. Tena hapa nchini ingelikuwa ni rahisi zaidi kwa JK kwani hakuna umwagaji wa damu katika wananchi kudai haki zao za kimsingi zaidi ya ukatili wa polisi ambao anayo mamlaka ya kuwakemea na wala hana mpango wa kufanya hivyo..

d) Katika kero za Muungano, JK aliwahi kudiriki kusema kamati ya kushughulikia kero tajwa na kuundwa na chama kimoja tu cha CCM wawe wanakutana angalau mara nne kwa mwaka hata kama hawana la kujadili ikimaanisha tu yeye JK anacheza mchezo wa siasa wa kuonyesha raia kazi inafanyika hata kama hakuna linaloendelea! Mbali ya hilo, JK hana mkakati wa kuzimaliza kero za Muungano nje ya CCM na ndiyo maana hawezi kufiria muundo mbadala wa kutafuta ufumbuzi wa kero za muungano nje ya chama chake sasa iwaje amtarajie Kagame atafute ufumbuzi wa kero za Rwanda nje ya chama chake cha RPF?

e)
JK hana taswira ya kuutetea na kulinda utawala bora na ndiyo maana katika kipindi chake mauaji yanayofanywa na polisi hadi leo yanazidi yale yaliyofanywa na maraisi wote waliomtangulia. Pia, katika historia ya nchi yetu kamwe Waziri Mkuu hajawahi kutamka hadharani kuwa ni sahihi kwa polisi kupiga raia wanaodai haki zao. Hadi wa leo, JK yuko kimya na wala hajamchukulia Pinda hatua yoyote ile ikiashiria anaafiki udhulumaji wa haki za kimsingi kabisa za binadamu! Hivi kwa kisa kipi Kagame amsikilize JK ambaye hana rekodi yoyote ile ya kuheshimu utawala bora?

2)
Chaguzi ya Uraisi 2010 kuna utata mkubwa kati yake na Dr. Slaa ni nani alishinda Uraisi kutokana na Tume ya uchaguzi kufanya kazi kwa minajili ya kulinda masilahi ya CCM huku ikishirikiana na Idara ya Usalama pamoja na serikali za mitaa. Kagame pamoja na faulo zake kibao, hakuna anayemtilia mashaka ya uhalali wa chaguzi zote zilizomsimika madarakani. Kwenye mazingira ya namna hii, ni JK au Kagame ambaye anastahili kuwekwa darasani na mwenzie juu ya utawala bora?

3) Viongozi wengi wa TZ hususani CCM hukimbilia kutatua matatizo ya nje ya chi yetu na kutumia sarakasi hizo kufunika matatizo ya hapa nchini lakini wasichojua ni kuwa ili waheshimike ndani na nje ya mipaka ya nchi hii ni pale watakapoanza kutatua kwa dhati matatizo ya hapa ndani na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu bila ya kujali masilahi ya muda mfupi ya vyama vyao.

4) Kwa karata hizi ni dhahiri Kagame yuko sahihi kabisa kumbeza JK kwa kumtishia na kunuia kumzabua kofi kwa kile ambacho ni
"kiherehere" cha JK kujiingiza katika tanuru la moto la wengine wakati hapa nyumbani moshi unafukuta kila mahali na JK haonyeshi hata dalili kujua majibu ya kero zetu yako katika nyanja ipi.