Posted by Unknown
Posted on Monday, August 26, 2013
Mchawi hivi karibuni kaleta kizaa zaa huko Dzivarasekwa alipokutwa na 'birthday suit' yake(uchi)
Sabina
Rokuzhe alikiri kuwa yeye ni mchawi na amedondoka alipokuwa anaruka
kwenye ungo akitokea kwenye trip yake ya kuloga huko Masvingo.
Alikutwa
kwenye nyumba ya Mbuya Annah Kamupaundi. Akaanza kuwaomba watu
waliomzunguka wasimpige ,akasema pia katembelea nyumba kadhaa katika
eneo hilo.
Mmoja wao aliyemuona asubuhi mapema ni Mrs Alice Hundi (37)
ambae alisema aliamka baada ya kusikia mayowe ya mwanamke kwenye saa nane hivi usiku.
"Nilipomuona
yuko uchi,nilimmwagia chumvi usoni, akaanguka na kuanza kujizungusha
zungusha chini. Tuliita polisi na akachukuliwa"
Polisi walitoa uhakika kwamba amechukuliwa na atapewa msaada wa psychiatric