muhtasari

Home » » Mwanawe Gbagbo atoa wito wa amani

Mwanawe Gbagbo atoa wito wa amani




Michel Gbagbo
Mwana wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo amesema kuwa anataka amani na maridhiano katika taifa hilo.
Michel Gbagbo ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu alikamatwa akiwa na babaake miaka miwili iliopita baada ya matokeo ya uchaguzi nchini humo kukumbwa na utata na kupelekea ghasia zilizosababisha maafa ya zaidi ya watu elfu 3.
Katika mahojiano na mwandishi wa BBC,baada ya kuachiliwa huru amesema kuwa mashtaka dhidi ya familia yake yalichochewa kisiasa.
Babaake Laurent yuko katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC akikabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Takriban watu 3,000 waliuawa katika ghasia za kisiasa baada ya Laurent Gbagbo kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu wa Novemba 2010 aliposhindwa na kisha kuondolewa mamlakani mwaka uliofuata kwa usaidizi wa wanajeshi wa Ufaransa na umoja wa mataifa yakimuunga mkono Alassane Ouattara.
Ni rais wa kwanza wa zamani kufikishwa mbele ya mahakama ya ICC kwa tuhuma za mauaji ya watu kwa msingi ya kisiasa ingawa anasisitiza kuwa hana hatua.
Michel Gbagbo, aliyezungumza na mwandishi wa BBC mjini Abidjan ambako aliweza kupatana na familia yake baada ya miaka wimili gerezani, alisema kuwa babake yu bukheri wa afya na anatarajia kuzungumza naye hivi karibuni.
chanzo:BBC

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger