Mabingwa wa Vodacom Premier League 2012 -2013, jana tarehe 10 Agosti
2013 wamezinduwa Tawi la Klabu hiyo kongwe lililooko Mbagala Kiburugwa
Mfenesini.
Kaimu Mkurugenzi wa Yanga, Ndg Denis Oundo akipandisha bendera ya Young
Africans Sports Club (Yanga) katika ofisi za Tawi hilo kuonesha
kuhitimisha ufunguzi wa Tawi. Bw. Oundo alimwakilisha Mwenyekiti wa
Klabu hiyo Ndg. Yusuf Manji.
WANACHAMA WAPYA
Baadhi ya wanachama wakipokea kwa furaha kadi zao mpya za uanachama
UJIRANI MWEMA – WATANI WA JADI WALISHINDWA KUJIZUIA …
JAMANI, USHINDI, RAHAAA….
Mwanachama akidhihirisha utamu ushindi kwa kulibusu kombe wana- Jangwani hao walilonyakuwa katika msimu wa 2012-13