Home »
KIMATAIFA
,
MICHEZO
» RAISI WA BARCELONA: MCHEZAJI YOYOTE ANAWEZA KUUZWA LAKINI SIO LIONEL MESSI - LABDA KWA ADA YA UHAMISHO WA €580 MILLIONI"
RAISI WA BARCELONA: MCHEZAJI YOYOTE ANAWEZA KUUZWA LAKINI SIO LIONEL MESSI - LABDA KWA ADA YA UHAMISHO WA €580 MILLIONI"
Posted by Unknown
Posted on Monday, August 05, 2013
Raisi wa Barcelona Sandro Rosell amesema klabu yake kamwe haitoweza kumuuza Lionel Messi, na alipoulizwa kama ni bei gani ambayo inaweza kubadilisha uamuzi wa klabu ajibu kwa kifupi tu "€580 million".
Akiongea katika mahojiano na gazeti la Sport.es, Sandro Rosell alisema: “Wachezaji wote wanaweza kuondoka ikitokea tumepata ofa nzuri yenye tija kwetu lakini sio Messi. Labda tulipwe kiasi cha €250 million ($332 million) kama ada yetu, pamoja na asilimia 56 ya fedha hizo kwa ajili ya kulipa kodi. Hivyo itabidi alipe kiasi cha €580 million.”
Kwa maana hiyo ili kumsajili Lionel Messi itabidi klabu inayomtaka ilipe fedha ambazo ingeweza kununua vilabu viwili kama Fulham - ambayo ilinunuliwa na billionea a kimarekani Shahid Khan kwa ($230 million).
Pia kwa kauli hiyo ya Rossell inaonekana FC Barcelona wapo tayari kumuuza mchezaji yoyote kwenye kikosi chao ikiwemo Cesc Fabgregas anayetakiwa na United ikiwa tu watapewa ofa itakayowaridhisha.