
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk Terezya
Huvisa ametangaza leo kuwa Serikali imepiga marufuku ungizaji,
utengenezaji, uuzaji, na utumiaji wa mifuko ya plastiki.
Zuio hili linahusu mifuko yote ya plastiki ya kubebea bidhaa kutoka madukani, sokoni na majumbani.
Mifuko
inayoruhusiwa ni ile yenye unene wa maikroni mia moja inayooza
(bio-digradable) na vifungashio vya bidhaa mbalimbali kama vile vifaa
vya mahospitalini.
“Marufuku hii inapaswa kuzingatiwa na wenye
viwanda, wenye maduka na wananchi kwa ujumla ili kutokomeza kuenea kwa
taka zinazotokana na mifuko ya plastiki kwenye mazingira,” amesema
Waziri.
Ametoa agizo la kufanywa msako ili
kuwakamata watakaokuwa wanaendelea kufanya biashara ya mifuko hii na
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amesema
kuwa Serikali imechukua hatua hii ili kupunguza naa kuondoa kabisa
tatizo la kusambaa na kutapakaa kwa taka za mifuko ya plastiki ambayo
baada ya matumizi huishia kuyachafua mazingira.
Imeelezwa
kuwa madhara yanayosababishwa na mifuko ya plastiki ni pamoja na
uharibifu wa udongo unaotokana na kuunguzwa kwa plastiki hizi na hivyo
kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama, kutooza kiurahisi
wa njia za kiasili (non-biodegradable) kuzagaa katika mito, maziwa,
bahari na nchi kavu hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai.