Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen.
Na Khatimu Naheka
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen, amepata gari jipya lenye hadhi yake.
Kocha huyo raia wa Denmark, alikuwa na mikasa mingi ya magari aliyokuwa akiyatumia, ambayo mengi yalikuwa na matatizo makubwa kiasi cha wakati mwingine kuharibika njiani.
Mara ya mwisho alikuwa akitumia gari aina ya Rav 4, ambalo awali lilikuwa likitumiwa na katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela.
Kufuatia usumbufu huo, hivi karibuni Championi Jumatano lilimnasa Kim akiwa na gari jipya kabisa aina ya Ford Everest lenye thamani ya Sh milioni 78, likiwa ndilo ghali zaidi kutumiwa na makocha wa nchini.
Uchunguzi uliofanywa na Championi Jumatano umebaini kwamba, katika makocha wa klabu za ligi, anayemfuatia Kim kwa kutumia gari la gharama ni Hemed Morocco wa Coastal Union, mwenye Land Rover Freelander linalouzwa Sh milioni 50.
Nafasi ya tatu inashikiliwa na Kocha wa Yanga, Ernie Brandts na yule wa Azam FC, Stewart Hall, wanaotumia magari aina ya Toyota Prado yenye thamani ya Sh milioni 38, kila moja.