muhtasari

Home » , , » MKUU WA WILAYA YA URAMBO MHESHIMIWA ANNA MAGOWA AMEFARIKI DUNIA...

MKUU WA WILAYA YA URAMBO MHESHIMIWA ANNA MAGOWA AMEFARIKI DUNIA...

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mheshimiwa Anna Magowa amefariki dunia. Imeelezwa kuwa, Mheshimiwa Anna Magowa aliondoka kwenye kituo chake cha kazi akiwa na hali mbaya kwa gari la wagonjwa hadi Tabora ambapo alipanda ndege kuelekea Dar-es-salaam kwa matibabu zaidi siku ya jumapili ya tarehe 15 Septemba, 2013. Jina la hospitali aliyopelekwa halijapatikana. Mheshimiwa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo wa muda mrefu hadi mauti yalipomfika.

Mheshimiwa Anna Magowa ( Mkuu wa Wilaya ya Urambo) enzi za uhai wake. Hapa ilikuwa ni siku ya mei mosi ya mwaka 2013.
Urambonews inawapa pole wanafamilia, ndugu, jamaa, marafiki na watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Marehemu.
-mbonde tz

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger