muhtasari

Home » , » HOTUBA ZA NYERERE LIVE KUSIKIKA KWENYE SIMU...

HOTUBA ZA NYERERE LIVE KUSIKIKA KWENYE SIMU...




·     
TAASISI ya Mwalimu Nyerere Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Push Mobile, imezindua teknolojia ya kuwezesha Watanzania kusikiliza na kuangalia hotuba za Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere kupitia simu za mkononi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Joseph Butiku alisema wameamua kuanzisha mpango huo, kuwawezesha Watanzania, Waafrika na dunia kujua kazi alizozifanya marehemu Baba wa Taifa kwa jamii.
Butiku alisema ili kupata hotuba hizo kupitia simu ya mkononi, unatakiwa kutuma neno Hotuba kwenda namba 15678 .
Vile vile, unaweza kupata picha nyingi zaidi kwa kuingia www.simu.tv/nyerere mobile tv. Alisema mpango huo upo kwa njia ya CD na DVD, ambazo Watanzania wengi wameanza kuzichangamkia kupata nakala.
“Huu ni mpango maalumu wa kuhakikisha kumbukumbu za marehemu Baba wa Taifa zinapatikana kiganjani na muda wowote, tumeingia makubaliano maalumu na Kampuni ya Push Media Mobile ili kuendeleza juhudi hizi za kuenzi enzi zake,” alisema Butiku.
Alisema Mwalimu amefanya kazi kubwa za kuelimisha kwa kutunga vitabu mbalimbali, ambavyo vingi vimekuwa vikutumika kusaidia mambo mbalimbali ya kisiasa na uchumi.
“Nakumbuka alisema kuwa mawazo haya yapo kwenye vitabu na kanda mbalimbali, yatumike katika kuchangia maendeleo ya binadamu, alikuwa mwangalifu sana kwani yamezingatia hali halisi ya jana na leo, natoa ushauri kwa Watanzania kutumia mpango huu ili kusaidia Taifa,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie Manento alisema wameingia makubaliano na Taasisi ya Mwalimu Nyerere lengo kubwa ni kurahisisha kupatikana busara za Mwalimu kwa Watanzania wote, ikiwa pamoja na vizazi vya sasa.
-Habarileo

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger