Mimi Samson Mwigamba, mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ninawasilisha malalamiko yangu kwa Msajili wa vyama na ninaomba atoe mwongozo kuhusu mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chama kufuatia kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.
Katiba ya Chadema ya mwaka 2004 kipengele 5.3.2 (c) inasomeka ifuatavyo kuhusu Muda wa Uongozi:
Kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja.
Hata hivyo katiba ya chama ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c) inayozungumzia muda wa uongozi inasoma:
Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimizamasharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimizamasharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Sentensi
kuhusu ukomo wa uongozi haipo. Ni kweli kuwa Marekebisho ya Katiba
yalifanyika mwaka 2006, lakini hoja ya kubadili kipengele hicho
haikuwepo na muhtasari zinaonyesha
wazi kuwa kulikuwa hakuna mjadala wa kipengele hicho au kuhusu suala
zima la ukomo wa uongozi.
Hivyo napenda nisisitize kuwa si kweli kwamba Chadema haijawahi kuwa
na Katiba ambayo ina ukomo wa uongozi.
Pia si kweli kwamba mwaka 2006
Katiba mpya iliandikwa upya bali marekebisho yalifanywa kwa baadhi ya
vipengele. Ila kipengele 5.3.2 (c ) haikujadiliwa.
Natumaini kuwa Msajili wa vyama ataweza kutupatia hekima zake na
kutoa mwongozo ili suala hili lipatiwe suluhisho la kudumu ndani ya
chama chetu.