muhtasari

Latest Article Get our latest posts by subscribing this site

LULU:" MIMI SIJACHUMBIWA KUOLEWA KUPO TU...TENA MIMI MDOGO"...

 
Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha fununu zilizoandikwa kwenye gazeti la udaku liitwalo ‘Filamu’ kwamba amechumbiwa na muda mchache ataolewa.
 
Akizunguza jana  kwennye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muigizaji huyo wa Foolish Age, alisema hajachumbiwa na mtu yeyote ila ni magazeti ya udaku tu ndio yamekuwa yakiandika kile yanachojisikia.
 
“Mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote aliyenichumbia na kama itatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua, na ni mimi mwenyewe ndiye nitakaesema,” alisema mrembo huyo.
 
“Lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari kutoka kwenye chanzo gani, by the way kwaajili kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu anayejisikia kuandika anaandika ,anaamka anaandika, anaamka anandika. 
 "Kwa hiyo leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, kwa hiyo inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo, kwamba ‘leo Lulu tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe’, I don’t know.
 
“Kuchumbiwa, kuolewa,kuwa mke ni vitu ambavyo tumeumbiwa binadamu, vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa.” Lulu

Ney Lee kufanya listening party ya albam yake jijini Mbeya Nov 17...




Hitmaker wa ‘Umekwenda’ na ‘Nipe Muda’ NEY LEE anatarajia kufanya Listening party ya albam yake ambayo mpaka sasa hajaipa jina, November 17 mwaka huu akianzia nyumbani kwao, Mbeya.
 
Kwenye party hiyo, Super Nyota huyo atasindikizwa na Juma Nature. Akiongea na kipengele cha ‘Chumba Cha Sindano’ kupitia kipindi cha Kali za ‘Bomba cha Kituo’ ya Bomba FM, Mbeya Ney Lee alisema jina la albam hiyo itakuwa ni surprise kwenye uzinduzi huo.
 
Albam yangu mpaka sasa hivi sijajua itaiitwaje, lakini tayari albam yangu ipo inakuja naanza na Mbeya tarehe 17 nitakuwa Mbeya lakini siwezi kusema ni wapi kwa sababu bado ni mapema na vitu vyote tayari vimeshapangwa lakisi nafikiri soon nitawajulisha wote itakuwa sehemu gani,” alisema.
 
“Nitasindikizwa na JUMA NATURE kwa hiyo nikitu ambacho sasa hivi nipo katika mchakato wa kukifanya na ni kitu serious kabisa. 

"Nita-launch albam yangu mwezi wa 12 kwa hiyo watu watasikiliza nyimbo, na watu wataweza kupiga picha na mimi, kuongea na mimi, kuniuliza maswali mengi coz itakuwa friendly show kwa hiyo watu wengi waje waone wasikie kabla ya kununua kile watakachokinunua wawe wameshakisikia before,” aliongeza.
 
Kwahiyo nimeanza na Mbeya peke yao ambao wataweza kusikia nyimbo zangu kabla ya kununua albam(kwa msisitizo) ila sehemu nyingine nitauza kawaida tu, sitotaja jina mpaka siku ya show yenyewe.”
 
Kwenye albam hiyo yenye nyimbo nane, muimbaji huyo amewashirikisha wasanii kama Linex, Kala Jeremiah na Ally Nipishe.

"WEMA AKAMATWE HARAKA"...KAULI YATOLEWA NA MAHAKAMA...


Mahakama ya mwanzo Kawe jijini dar es salaam imetoa hati ya kumkamata miss tanzania 2006 Wema Sepetu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni dharau ya wito wa mahakama hiyo. 
 
Chanzo cha ndani kilichoomba kuhifadhiwa ya jina kimempasha mwandishi wetu kuwa hati hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya wema kushindwa kuhudhuria kesi yake iliyopo mahakamani hapo na bila kutolewa udhuru wowote. 

Aidha imeelezwa kwamba mahakama hiyo pia imetilia mashaka udhuru uliotolewa septemba 30 kwamba wema ni mgonjwa baada ya kuvuja kwa picha katika mitandao zikimuonyesha Wema akila bata  Hong Kong China na mpenzi wake wa zamani mwanamuziki Diamond. 

Wema alitolewa udhuru huo na kijana aliefahamika kwa jina la Martini .
 Kesi inayomkabili wema katika mahakama hiyo ni ya kumtukana matusi ya nguoni pamoja na kumpiga meneja wa hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe beach jijini Dar es salaam bwana Godluck kayumbu. 

Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi wetu alimtafuta mlalamikaji wa kesi hiyo bwana Kayumbu na kumuuliza kuhusu hati iliyotolewa na mahakama ambapo alithibitisha kuwepo kwa jambo hilo. 

Bwana Kayumbu alisema kuwa amepewa hati  maalum ya kumkamata wema octoba 30 mwaka huu ambayo kesi hiyo ilitajwa tena mahakamani hapo.
Alisema kuwa Wema Sepetu anaweza kukamatwa muda wowote kuanzia sasa kwani octoba 30 mwaka huu kesi hiyo ilitajwa tena mahakama ya Kawe chini ya mheshimiwa hakimu Ikanda lakini wema hakutokea na hakuna mtu yeyote aliyekuja kwaajili ya kumtolea udhuru.
Kayumbu alibainisha kuwa mshtakiwa wake wema sepetu hakuja mahakamani mara mbili mfululizo kuanzia septemba 30 2013 na kudaiwa kuwa anaumwa lakini picha zake katika mitandao zilimuonyesha  akitanua hong kong china na mara ya pili kesi hiyo ilitajwa octoba 30 2013 ambapo hakutokea mtu yeyote anayemuhusu wema katika mahakama hiyo. 

"Kesi ilikuwa ya kwanza kutajwa lakini nilikuwa peke yangu sasa nikaamuliwa mimi nipewe hati maalum ya kumkamata wema ambapo nilipewa na nimeshaikabidhi kituo cha polisi cha kawe kwa utekelezaji maana naona muda unazidi kwenda na kesi haiishi," alisema kayumbu.
Mwandishi  wetu alipomtaarifu bwana kayumbu kuwa octoba 30 Wema Sepetu alikuwa kwenye msiba baada ya kufiwa na  baba yake mzazi mzee Isaac Sepetu na kwamba siku hiyo alikuwa safarini kwenda zanzibar kwa ajili ya mazishi ya mzazi wake huyo, bwana kayumbu alisemaa kuwa suala hilo halimuhusu kwani hata yeye amefiwa na wazazi wake. 
"Kama kafiwa hata mimi nimefiwa na baba na mama yangu pia, kinachotakiwa ni kutii sheria za nchi ikiwemo mahakama ,kama alifiwa kwanini asitoe udhuru? sina mazungumzo tena kinachotakiwa ni sheria ichukue mkondo wake, popote atakapopatikana wema ni lazima akamatwe," alisema Godluck. 
Wema hakupatikana kwenye simu ili kuzungumzia jambo hilo.

-Gazeti  la  Kiu  toleo  la  leo.

MAKUBWA...MAHARI NDOGO, WAREMBO WA KINYARWANDA WASABABISHA WAHAMIAJI HARAMU NGARA...




 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta
ONGEZEKO kubwa la wahamiaji haramu wilayani Ngara mkoani Kagera linatokana na Watanzania kuamua kuoa wanawake wa Rwanda kuliko Watanzania kutokana na kutozwa mahari kidogo na kuvutiwa na uzuri wa wanawake wa Kinyarwanda, Imeelezwa.
Katika hatua nyingine Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ameahidi kuwasilisha ombi maalumu kwa Rais Jakaya Kikwete ili wanawake wa Rwanda waliokuwa wameolewa nchini na kukumbwa na Operesheni Kimbunga, warejee nchini kuungana na familia zao lakini kwa kuhalalisha ukaazi wao.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Constatine Kanyasu aliyekuwa akisoma taarifa ya utekelezaji wa Operesheni Kimbunga awamu ya kwanza iliyohusisha mpaka wa Rusumo unaozitenganisha Rwanda na Tanzania, alisema kumekuwepo na ongezeko kubwa la wanaume wa Tanzania kuoa wanawake wa Rwanda kutokana na udogo wa mahari na uzuri wa Wanyarwanda.
Alisema hata hivyo pamoja na kupendezewa na vitu hivyo kwa wanawake wa Kinyarwanda lakini wanaume hao wa Tanzania wanashindwa kuwalipia wake zao hao ada ya Dola za Marekani 550 ( Sh 880,000) zinazotozwa kila baada ya miaka miwili ili kuhalalisha ukazi wao nchini kutokana na kutobadili uraia kuwa Watanzania.
“Waziri (Sitta) sababu kubwa wanayoitoa wanaume wengi wilayani hapa (Ngara) kama sababu ya Watanzania wengi kuamua kuwaoa Wanyarwanda ni kutozwa mahari kidogo sana kuliko ile inayotozwa ili kumuoa mwanamke wa Tanzania. Inasemekana kuna familia wanapokea hadi kuku, mbuzi au fedha kidogo ili kuruhusu mtoto wao kuolewa.
“Kwa vile wanapenda kuwa na wake na kwa vile hawana uwezo wa kifedha wa kutoa mahari kubwa uamuzi wanaofikia ni kuoa wanawake wa Kinyarwanda, lakini kwa kufanya hivyo wanajikuta pia wanashindwa kuwalipia wake zao ada hiyo ya ukazi na kuwafanya kuishi nchini kinyume cha utaratibu,” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Alisema kutokana na hatua hiyo Operesheni Kimbunga imewakumba wanawake wengi waliokuwa wameolewa nchini hatua iliyosababisha kubakia kwa watoto wasiokuwa na mama wa kuwalea na inayozorotesha uhusiano wa kifamilia na mataifa ya Rwanda na Tanzania.
Alisema wakati maofisa wa Serikali wa pande hizo mbili walikuwa na kawaida ya kukutana kila baada ya miezi mitatu kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano na usalama, tangu kuanza kwa Operesheni Kimbunga vikao hivyo havifanyiki.
Akizungumzia kuondoka kwa wanawake walioacha familia zao, Waziri Sitta ambaye pia alikiri uzuri wa wanawake Wanyarwanda alisema atawasilisha pendekezo kwa Rais Kikwete ili waweze kuruhusiwa kurejea nchini na kufuata taratibu za ukazi halali ili kuweza kulea familia zao.
“Hatuna ubaya na watu wa Rwanda hata chembe na tunaomba walielewe hilo.Operesheni Kimbunga imewakamata pia Wahindi, Wamalawi, Wachina na hawa Wamakonde maana wapo Wamakonde wa Kusini mwa Tanzania lakini wapo Wamakonde wa Kaskazini mwa Msumbiji hawa pia wamekumbwa na operesheni hii.
“Ikumbukwe kwamba ni haki ya kila nchi kuendesha operesheni ya kuhakiki ukazi wa wahamiaji. Ila kwa sababu ya ujirani mwema na hasa kwa kuzingatia hili la wanawake kuacha familia zao nitapeleka mapendekezo kwa Rais tuweze kurekebisha maana tunabanwa pia na mikataba ya kimataifa inayohusu haki za binadamu na watoto,” alisema Sitta.
Akizungumzia malipo ya Dola 550 kila baada ya miaka miwili zinazopaswa kulipwa ili kuwezesha mke asiye raia kuishi nchini, Waziri Sitta alisema ni vizuri kiwango hicho kikaangaliwa upya kutokana na ukweli kwamba wanaume wengi wanaokimbilia Rwanda kuoa wanakwepa ukubwa wa mahari nchini Tanzania kwa kutokuwa na uwezo.
“Nadhani kuna umuhimu wa kuangalia upya kiwango hiki, maana kwa mtu asiye na uwezo kulipa ada hiyo tena kwa Dola ya Kimarekani kunaweza kuwa ni chanzo cha kukwepa sheria na taratibu za nchi yetu. Lengo si kuwafukuza wenzetu bali kuwataka wafuate sheria,” alisema.
Akizungumzia wahamiaji haramu waliorejeshwa makwao, Kamanda wa Uhamiaji Rusumo, Samwel Mahilane alisema hadi kufikia Oktoba mosi mwaka huu, wahamiaji haramu 7, 858 walirejea makwao kwa hiari kupitia mpaka wa Rusumo, huku wahamiaji 2,890 wakirejeshwa kwa nguvu na kufanya jumla ya wahamiaji waliorejea nchini Rwanda kufikia 10,348
-habarile

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger