Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametahadharisha kuwa kama tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana halitapatiwa ufumbuzi, itakuwa chanzo cha serikali kupoteza madaraka.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alisema hayo jana wakati akichangia mjadala wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2014/2015, uliowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira.
Lowassa alisema serikali inapaswa kuangalia kipaumbele muhimu na kinachowezekana kutekelezwa cha kuanzia na kufuatia kingine.
Alisema kama angekuwa yeye (Lowassa), angeanza na kipengele cha ajira. “Huwezi kuzungumza mipango bila kuzungumza habari ya ajira,” alisema Lowassa.
Alisema serikali inapaswa kukiri kwamba, kuna Watanzania wengi waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne na cha sita, walioko mitaani hawana ajira. Tusipoangalia watakuja kula sahani moja na sisi. Tusipowashughulikia,” alitahadharisha Lowassa.
Alisema iwapo serikali haitokuwa macho juu ya hilo na kulishughulikia, yale yanayotokea katika nchi mbalimbali barani Afrika, yanaweza pia kutokea hapa nchini.
Ingawa Lowassa hakufafanua maana ya kula sahani moja wala kutaja nchi za
Afrika ambazo zimesumbuliwa na vijana, Tunisia na Misri ni miongoni mwa
nchi zilizokumbwa na vuguvugu la mageuzi kiasi cha kusababisha watawala
kuondolewa madarakani.
Vijana kwa maelfu waliingia mitaani katika nchi hizo wakipinga hali
mbaya ya uchumi hasa kukosekana kwa ajira na mwishowe serikali
zilizokuwa madarakani ziliangushwa.
Lowassa alisema katika mkutano wa Benki ya Dunia (WB) uliofanyika
mwaka huu kulizungumzwa habari kuhusu mdororo wa kiuchumi uliolikumba
bara la Ulaya.
Alisema moja ya nchi zilizokumbwa na tatizo hilo ni Hispania, ambayo
alisema katika kujinasua, ilimbana kila mwekezaji aliyekuwa akiingia
katika nchi hiyo kwa kumpa sharti la kuwekeza ajira ya vijana.
Kwa mujibu wa Lowassa, mkakati huo uliisaidia Hispania, ambayo katika
miaka miwili mitatu iliyofuatia ilifanikiwa kujinasua kuondokana na
tatizo hilo.
“Lazima tuangalie suala la ajira, ni muhimu sana. Mipango mingine haiwezekani bila kutizama suala la ajira,” alisema Lowassa.
Alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwassa, na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, mkoani humo, Elibariki Kingu, ambao alisema wameanza kuhangaikia suala la ajira kwa vijana. Alisema iwapo kila wizara ikiamua kushughulikia suala la ajira kwa vijana linawezekana.
“Yule mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wameamua kuchukuwa vijana
waliomaliza Chuo Kikuu, wamewatafutia mashamba, wamewatafutia trekta.
Wale vijana wamefanya kazi nzuri sana. Kwa hiyo, inawezekana,” alisema
Lowassa.
Kadhalika, alisema mipango mingi ya maendeleo nchini imekuwa haifanikiwi
kutokana na serikali kutokuwa na msimamo wa kufanya maamuzi magumu.
Badala yake, alisema imekuwa ikiishia kupanga, lakini hakuna
utekelezaji na hivyo kuungana na wananchi kulalamikia kukwama kwa mambo.
Alisema anapongeza sana uamuzi wa serikali kuanzisha kitengo maalumu kilicho chini ya Ofisi ya Rais, kijulikanacho kama ‘Presidential Delivery Bureau’ (PDB), kinachosimamia mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na kusema: “Hongereni sana.”
Hata hivyo, akaitaka serikali kujiuliza maswali kama kitengo hicho kina ‘meno’ ya kufanya maamuzi magumu?
“Tatizo la nchi hii mnazungumza mambo hakuna utekelezaji. Tunazungumza,
lakini discipline (nidhamu) ya (nchi ya) Malaysia na hapa (Tanzania) ni
tofauti. Hapa kuna uswahili mwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo,
mnaamua hamtekelezi,” alisema Lowassa.
Alishauri kuwapo na chombo, ambacho kinaweza kufanya maamuzi magumu na yakawa magumu yanayotekelezeka kweli kweli. Alisema tabia ya kujivika joho la kufanya maamuzi ya utekelezaji, lakini bila kufanya, ni kazi bure.
Kwa hiyo, akasema uamuzi wa kuwa na PDB ni mzuri, lakini akasisitiza
kuwa usipoangaliwa itakuwa ni sawa kufanya kazi bure, hivyo akashauri ni
lazima kuwapo na meno ya kuuma.
“Tukikubaliana mambo yafanyike. Haiwezekani katika nchi kila mtu
akawa analalamika. Kiongozi analalamika, mwananchi analalamika, haiwezi
ikawa ni jamii ya kulalamika lalamika. Awepo mtu mmoja anayefanya
maamuzi na anayechukua hatua,” alisema Lowassa.
Alisema bila kuchukua hatua, kazi ya serikali na wananchi itabaki kuwa ya kulalamikiana.
Alitoa mfano wa uhasama uliopo baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC), akisema hakuna haja kwa Tanzania kugombana na
marais; Paul Kagame (Rwanda), Uhuru Kenyatta (Kenya) na Yoweri Museveni
(Uganda) kwa kuamua kushirikiana kiuchumi na Sudan Kusini na kuitenga
Tanzania.
Alisema kwani Tanzania inaweza kushirikiana na Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Goma, ambako alisema ni kuzuri zaidi ya
Sudan.
Lowassa alisema inachohitaji Tanzania kufikia hilo, ni kufufua reli ya kati ili kuzalisha kuliko nchi hizo.
VIPAUMBELE KATIKA MPANGO WA MAENDELEO
Kuhusu vipaumbele vilivyomo katika Mpango huo, alisema ni vingi na kushauri kwamba, vingechaguliwa vichache vikasimamiwa na kutekelezwa.
Kuhusu vipaumbele vilivyomo katika Mpango huo, alisema ni vingi na kushauri kwamba, vingechaguliwa vichache vikasimamiwa na kutekelezwa.
Alisema kupanga vipaumbele vingi kwa wakati mmoja ni vigumu kutekeleza vyote.
ELIMU
Alisema kipaumbele cha pili ambacho alishauri kipewe kipaumbele ni elimu. Lowassa alisema kinachozungumzwa juu ya elimu hakipaswi kupuuzwa na kusema lipo tatizo la msingi katika elimu ya Tanzania, kwani vitu vinavyochukuliwa havitoshelezi.
Alisema kipaumbele cha pili ambacho alishauri kipewe kipaumbele ni elimu. Lowassa alisema kinachozungumzwa juu ya elimu hakipaswi kupuuzwa na kusema lipo tatizo la msingi katika elimu ya Tanzania, kwani vitu vinavyochukuliwa havitoshelezi.
Alisema alitegemea kuwa Kamati ya Bajeti ingepata taarifa ya Waziri Mkuu
iliyotolewa juu ya elimu kama ingetambua baadhi ya matatizo, serikali
ikaangalia cha kufanya.
“Haitoshi kuchukua wanafunzi wengi wanaomaliza Chuo Kikuu wakati akienda
sokoni uwezo wake wa kimasomo haupo sokoni” alisema Lowassa.
Alisema hiyo inatokana na wanafunzi wengi wanaomaliza Chuo Kikuu
kutokuwa na hakika ya ajira kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa
kushindana katika soko.
Lowassa alisema kelele zinazopigwa na wananchi juu ya elimu nchini,
inafaa ukafanyika mjadala kuangalia tatizo lililopo katika elimu na nini
cha uhakika cha kufanya.
Alisema vinginevyo serikali isipoangalia, Tanzania itaachwa nyuma na
EAC, Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na dunia
kwa jumla, badala yake itabaki kuwa mbabaishaji katika soko la elimu.
“Tuwasaidie vijana wetu, tubadilishe mfumo wa elimu, tuangalie tunaweza kufanya nini vizuri zaidi,” alisema Lowassa.
AMSIFU WAZIRI MAGUFULI
Alisema kipaumbele cha tatu kwa maoni ni reli ya kati na kwamba, anamsifu sana Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa kazi nzuri ya ujenzi wa barabara aliyoifanya.
Alisema kipaumbele cha tatu kwa maoni ni reli ya kati na kwamba, anamsifu sana Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa kazi nzuri ya ujenzi wa barabara aliyoifanya.
Lakini akasema barabara hizo zimeanza kuharibika kwa kasi ya hali ya juu
sana. “Tumetoka Singida juzi, barabara imeharibika vibaya sana. Ile ya
Shinyanga, imeharibika vibaya sana. Kwa sababu malori yanayokwenda
yanayopasa kutembea kwenye treni yanatembea kwenye barabara…Naomba reli
ya kati muiangalie kwa haraka sana,” alisema Lowassa.
FOLENI DAR, AMSIFU WAZIRI MWAKYEMBE
Akizungumzia tatizo la foleni jijini Dar es Salaam, kwanza alimpongeza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na tatizo hilo.
Akizungumzia tatizo la foleni jijini Dar es Salaam, kwanza alimpongeza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na tatizo hilo.
Hata hivyo, alisema jitihada hizo za Waziri Mwakyembe pekee hazitoshi,
kwani muda wa saa ambazo wakazi wa Dar es Salaam wanaoupoteza kwenye
foleni zikipangwa kwa ajili uzalishaji ni nyingi sana.
Kwa hali hiyo, alisema serikali haiwezi kukaa hivi hivi, kwani hiyo ni hatari kwa uchumi wa nchi.
“Mtafute njia ya kuangalia tunafanyaje foleni ya Dar es Salaam, sasa si
kungoja, it has to be done now (inatakiwa kufanyika sasa),” alisema
Lowassa.
MBUNGE AMUUNGA MKONO
Mbunge wa Pangani (CCM), Saleh Pamba, akichangia mjadala huo, alimuunga mkono Lowassa, kwa kusema urasimu uliomo serikalini ni wa kuchukua maamuzi na kusema kwa mwenendo huo kamwe nchi haiwezi kuendelea. Alisema Malaysia wamefanikiwa na kupiga hatua katika maendeleo kwa sababu kuu moja tu ya kuchukua maamuzi kwa haraka.
Mbunge wa Pangani (CCM), Saleh Pamba, akichangia mjadala huo, alimuunga mkono Lowassa, kwa kusema urasimu uliomo serikalini ni wa kuchukua maamuzi na kusema kwa mwenendo huo kamwe nchi haiwezi kuendelea. Alisema Malaysia wamefanikiwa na kupiga hatua katika maendeleo kwa sababu kuu moja tu ya kuchukua maamuzi kwa haraka.
CHANZO:
NIPASHE