Na Baraka Mbolembole
Timu ya Taifa ya Kenya ' Harambee Stars', leo itakata ' utepe' wa
michuano
ya Mataifa ya ukanda wa CECAFA, kwa kucheza na timu ya Taifa ya
Ethiopia. Wenyeji hao wa michuano ya sasa na makamu bingwa wa taji hilo,
wanapewa nafasi kubwa ya kuvuka kundi A, mbele ya Ethiopia,
Zanzibar, na Sudan Kusini.
Mabingwa
watetezi, Uganda wao wapo kundi C, pamoja na Rwanda, Sudan, na Eritrea
katika kundi linalotarajiwa kuwa gumu zaidi katika michuano hiyo. Moi
Kasarani na Nyayo Stadium, ni viwanja viwili vilivyopo
katika jiji la Nairobi, Kisumu Stadium, Mombasa, na Machakos ni idadi
ya
viwanja vitano ambavyo vitazipokea timu 12. Mapema leo mchana
wawakilishi wengine wa Tanzania, timu ya Zanzibar Heroes itacheza na
Sudan Kusini katika mchezop wa kwanza kabisa mwaka huu.
KILIMANJARO STARS vs ZAMBIA
Timu
ya Taifa ya Tanzania Bara itaanza kibarua chake cha kwanza siku ya
kesho, Alhamis kwa kucheza na timu ' alikwa' ya Zambia katika mchezop
unaosubiliwa kwa hamu na wapenzi wa soka. Zambia, mabingwa wa michuano
ya Mataifa ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika, COSAFA, iliifunga Kilimanjaro
Stars katika mchezo wa mwisho kukutana katika michuano hii,
walipoalikwa kwa michuano iliyofanyika, Dar es Salaam, 2010.
Mbele
ya Rais wa Jamhurio ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete,
Stars ilipoteza kwa kulala bao 1-0 siku ya ufunguzi. Disemba mwaka
uliopita, Taifa Stars iliifunga timu ya Zambia kwa bao 1-0 katika mchezo
wa kimataifa wa kirafiki huku ' Chipolopolo' wakiwa na nyota wao
waliotwaa taji la mataifa ya Afrika, februari, 2012.
STARS, MATUMAINI YOTE KWA NGASSA
Moja
kati ya silaha za hatari katika michuano hiyo ni kiungo mshambuliaji,
Mrisho Ngassa. Ni mchezaji ambaye huvuta hisia kubwa za mashabiki hasa
timu yake inapokuwa nje ya Tanzania, kasi, ujanja, unyumbulifu, na
kucheza kwa kuhaha sehemu kubwa ya uwanja ni sifa ambazo zinampa nafasi
ya kipekee kutamba katika michuano hii.
Wakati,
kocha wa Stars itambidi asubiri hadi mapema mwezi ujao kupata huduma za
washambuliaji wake wawili, kati ya watatu katika safu ya mashambulizi,
Mbwana Samatta na Tomas Ulimwengu, ambao watakuwa na mchezo wa marejeano
wa fainali ya kombe la shirikisho Afrika, wikiendi hii wakiiwakilisha
klabu yao ya TP Mazembe, Kim Poulsen atamtegemea mfungaji huyo bora wa
michuano iliyopita nchini Uganda.
Elius
Maguli, Juma Luizio, Joseph Kimwaga, na Amri Kiemba wawili kati yao
wanataraji kuanza sambamba na Ngassa katika safu ya mashambulizi.
Itakuwa ni nafasi nzuri kwao na pengine kijana Said Dilunga anaweza
kufanya vizuri zaidi yao kama atapewa nafasi ya kutosha.
Katika
nafasi ya kiungo, KIM, bado anao wachezaji ambao wana uwezo na uzoefu
wa kutosha, SAlum Abubakary atakuwa akicheza michuano yake ya pili,
sambamba na Frank Domayo na wawili hao waliweza kucheza vizuri japo
waliambulia nafasi ya nee baada ya kufungwa na Zanzibar katika mchezo wa
kutafuta mshindi wa tatu. Kwa upande wa uzoefu itakuwa ni pigo kubwa
kwa Stars kama wachezaji hao vijana watashindwa kuendena na michuano kwa
kigezo cha uzoefu wao mdogo. Ni vijanma ambao wameshikilia namba katika
vilabu vyao vya Azam FC, na Yanga kwa zaidi ya miezi 14 sasa, na
wamekuwa chaguo la kwanza katika michezo zaidi ya 15 ya Kilimanjaro
Stars, na Taifa STars katika kipindi cha mwaka mmoja sasa
Wanatakiwa
kujiam,ini zaidio na kuongeza uimakini katika mchezo dhidi ya Zambia,
timu ambao husifika kwa kasi yao mchezoni na mchezo wa pasi za haraka
haraka zile fupifupi, Kwa, Salum sina shaka ataweza kuwazima kama ilivyo
kawaida yake, ni mtaalamu wa pasi fupi na ndefu, ni nadra kupoteza au
kupiga pasi ' fyongo' uwanjani, wakati Domayo akisifika kwa utulivu
wake, bado viongo hao wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la kushindwa
kutengeneza nafasi za mwisho japo muda mwingine huoneka kumiliki mchezo
kwa kiasi kikubwa.
Wakati,
Samatta na Ulimwengu tukisubiri huduma zao silaha yetu kubwa sasa ni
Ngassa, ni vipi tunaweza kumchezesha na akaisadia timu, mbio zake, akili
yake na uwezo wake alionao wa kutambua afanye nini atapokuwa amefika
katika lango la adui, Domayo anaweza kupiga pasi ndefu zilizotimilifu
itakuwa vyema kumtumia huyu kupiga pasi za haraka kwa Ngassa. Ni wazi
Zambia watamili mpira mpira hiyo ni kutokana na namna tunavyoshindwa
kuwa mashindanoni. Kwa nini nasema hivyo? Wakati mwingine ni lazima tuwe
wazi wachezaji wetu hutuangusha hasa pale tunapokuwa tunaweka imani
kubwa juu yao.
Kufungwa
michezo mitatu, kati ya sita katika michuano iliyopita ni sawa na kutoa
udhibitisho huo, wakati tulipofungwa mchezo wa kwanza na Burundi,
ilitukumbusha kupandisha kiwango chetu cha uchezaji, hiyo ilitusaidia
hadi kuwa na wafungaji bora wawili siku ya mwisho wa michuano. Tulicheza
vizuri katika michezo miwili tu iliyofuata, lakini kipigo kutoka kwa
Uganda kilikuwa ni ' kizito sana' katika vichwa vya mashabiki wa soka
nchini. Tulifungwa kidhaifu sana katika mchezo wa nusu fainali huku
Watanzania wakiamini kuwa ilikuwa nafasi yetu kuvunja utawala wa zaidi
ya miaka kumi wa Uganda kutofungwa nyumbani.
Uzoefu
wa wachezaji kama Kelvin Yondan, Athumani Idd ' Chuji' , Kiemba,
Ngassa, Erasto Nyoni, Ivo Mapunda, usiishie katika uwakilishi wa
uwanjani tu, wanatakiwa kuwakumbusha wachezaji vijana kama kina
Ramadhani Singano, Domayo, Dilunga, Kimwaga na wengine umuhimu wa kuona
fahari kushinda mataji wakiwa katika jezi ya taifa. Wakati tulipopata
taji la mwisho mwaka 2010 kuna vijana ambao walitoka mitaani na kupata
nafasi ya kukutana na watawala wa juu wa nchini. Ni fahari kuichezea
timu yako ya Taifa. Ila mafanikio ndiyo kipimo sahihi cha ubora wa jambo
lolote. HIvyo wachezaji wanatakiwa kufahamu kuwa tangu kizazi na kizazi
wapo wachezaji ambao wamekuwa wakiiwakilisha nchi, ila wale
waliofanikiwa kushinda chochote ndiyo waliopata nafasi ya kufika
bungeni, ikulu na sehemu nyingine ambazo si rahisi kufika.
KUJIAMINI KUPITA KIASI
Japo
umakini limekuwa tatizo kubwa kwa Stars, kujiamini kupitiliza imekuwa
ni sumu ambayo imekuwa ikituangamiza sisi wenyewe. WAtazame, Salum,
Domayo na safu ya ulinzi. JInsi wanavyokuwa wanacheza wakati tukimiliki
mpira imekuwa kama hawajui umuhimu wa kutengeza nafasi za kufunga mabao.
Hii ni michuano ya mtoano. Nafasi moja, bao moja, kufungwa inamaanisha
kuwa mchezo ujao utakuwa ni mgumu kuliko kama mngeshinda, na nafasi
inakuwa ndogo ya kusawazisha mambo.
Safu
ya ulinzi, Nyoni, anatakiwa kupevuka kiuchezaji sasa na kuacha na soka
la ' kipima joto', huwa hatabiriki , ingawa akiwa katika siku yake nzuri
utapenda kuona anavyokuwa akiisaidia timu katika mashambulizi na
kuzuia, ila akiwa hovyo utatamani apasi, akisumbuliwa mara mbili au tatu
hupoteza kujiamini na umakini wake unakuwa chini zaidi. Kwa kifupi safu
za ulinzi wa pembeni zikiwa imara na kufanya kazi ipasavyo hufanya
ulinzi wote kuimarika, ila wakiwa katika kiwango cha kupoteza mipira
hovyo na kushindwa kujiamini katika maamuzi yao hupelekea kuvuruga mambo
na wakati walinzi wa kati wakishirikiana na viungo kujaribu kuweka
mambo sawa mara nyingi tunajikuta tukipotea kabisa uwanjani. Wachezaji
wa ulinzi watakiwa kucheza soka lililokamilika kwa wakati huu wakiwa na
michezo mingi katika historia yao.
"
Kama utacheza vizuri na kushinda hilo ni bora, ila kama hautocheza
vizuri kwa namna yoyote ile, hakikisha ushanda kwa namna yoyote"
aliwahi kusema, Luis Aragones, kocha wa kwanza kuipa Hispania taji baada
za kupita miaka zaidi ya 40.
BURUNDI, UGANDA, ETHIOPIA
Stars
itacheza tena na Burundi katika kundi la B, na matokeo yao dhidi ya '
Risasi za Shaba' hapo kesho yanaweza kuufanya mchezo dhidi ya makamu
bingwa hao wa mwaka 2004 kuwa mgumu zaidi na kuamua hatma ya kundi.
Mwaka jana bao lililofungwa na Suleimani Ndikumana lilizamisha Stars
nchini Uganda katika mchezo wa hatua ya makundi. Burundi, sambamba na
Uganda, na Ethiopia wanaitumia michuano hii ili kujiweka sawa na
michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani,
CHAN 2014, nchini Afrika ya Kusini, mapema mwaka ujao.
TAKWIMU
Hizi ni takwimu za kila nchi katika michuano hiyo tangu kuanzishwa.
Namba ni nafasi ambayo timu huonesha ilimazima katika nafasi gani
1'
Huonesha ni nafasi ya kwanza, Namba mbili huwakilisha nafasi ya pili,
Namba tatu kwa nafasi ya tatu kama ilivyo kwa namba nne kwa nafasi ya
nne.
Burundi
1 –
2 2004
3 –
4 1999, 2007, 2008
Ivory Coast
1 –
2 2010[b][i]
3 –
4 –
Eritrea
1 –
2 –
3 –
4 1994
Ethiopia
1 1987, 2001, 2004, 2005
2 –
3 2000
4 1995, 2010
Kenya
1 1975, 1981, 1982, 1983, 2002
2 1979, 1985, 1991, 1999, 2001, 2008, 2012
3 1978, 1988, 1989, 1994, 1995, 2003
4 1977, 1984, 1996, 2004
Malawi[i]
1 1978, 1979, 1988
2 1975, 1984, 1989
3 1977, 1980, 1985
4 1983, 1992
Rwanda
1 1999[b]
2 2003, 2005, 2007, 2009, 2011
3 1999, 2001, 2002, 2006
4 2000, 2001[b]
Sudan
1 1980, 2006, 2007
2 1990, 1996[b]
3 1996, 2004, 2011
4 1991, 2003
Tanzania
1 1974, 1994, 2010
2 1973, 1980, 1981, 1992[b], 2002
3 1979, 1990, 2008
4 2009, 2011, 2012
Uganda
1 1973, 1976, 1977, 1989, 1990, 1992, 1996, 2000, 2003, 2008, 2009, 2011, 2012
2 1974, 1982, 1994, 1995[b], 2000
3 1983, 1984, 1987, 1991, 2007, 2010
4 1978, 1981, 1985, 2002, 2005, 2006
Zambia[i]
1 1984, 1991
2 1976, 1977, 1978, 1988, 2006
3 1981, 1992
4 1980, 1989
Zanzibar
1 1995
2 –
3 2005, 2009, 2012
4 1979, 1982, 1987, 1990
Zimbabwe[i]
1 1985
2 1983, 1987
3 1982
4 1988
By number of titles won and editions participated in
Team 1ST 2ND 3RD 4TH Pld Pldlst
Uganda 13 5 6 6 35 2012
Kenya 5 7 6 4 34 2012
Ethiopia 4 – 1 2 17 2012
Tanzania 3 5 3 3 33 2012
Malawi 3 3 3 2 21 2012
Sudan 3 2 3 2 19 2012
Zambia 2 5 2 2 20 2010
Zimbabwe 1 2 1 1 16 2012
Zanzibar 1 – 3 4 32 2012
Rwanda B 1 – – – 2 2001
Rwanda – 5 4 2 16 2012
Burundi – 1 – 3 13 2012
Côte d'Ivoire B – 1 – – 1 2010
Eritrea – – – 1 10 2012
Djibouti – – – – 10 2011
Kenya B – – – – 2 1994
Seychelles – – – – 2 1994
Somalia – – – – 23 2012
South Sudan – – – – 1 2012
Sudan B – – – – 1 1996
Tanzania B – – – – 1 1992
Uganda B – – – – 2 2000
Zimbabwe U23 – – – – 1 2