muhtasari

Home » , , » SERIKALI YABARIKI TANESCO KUPANDISHA BEI ZA UMEME...WAZIRI ADAI KUWA ATAKAYESHINDWA KUMUDU GHARAMA HIZO BASI ATUMIE KIBATARI...

SERIKALI YABARIKI TANESCO KUPANDISHA BEI ZA UMEME...WAZIRI ADAI KUWA ATAKAYESHINDWA KUMUDU GHARAMA HIZO BASI ATUMIE KIBATARI...

 Naibu Waziri wa umeme, Mh George Simbachawene, amesema kwamba serikali imekubali TANESCO waongeze gharama za umeme kwa 68% kama walivyokuwa wameomba.
 
Simbachawene ameitoa  kauli hiyo wakati akiongea katika kipindi cha Kumepambazuka kupitia Radio One leo asubuhi. 


Amesema kwamba hata kama TANESCO wakiongeza gharama za umeme hadi kufikia Tsh 800 kwa unit bei hiyo ni nafuu kuliko gharama za kununua mafuta ya taa.
 
Mh Simbachawene ametahadharisha kwamba kama mtu ataona kwamba gharama za umeme ni kubwa, basi akawashe kibatari au akae gizani.
 
Source: Jamiiforum  via Kumepambazuka, Radio One.

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger