![]() |
| Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema |
Latest Article Get our latest posts by subscribing this site
MAKUBWA: MWANAMKE AJIMALIZA KWA KUTUMIA MTANDAIO WAKE MWENYEWE...
Posted by Unknown
Posted on Monday, November 11, 2013
"NATAFUTA MWANAUME MWENYE MAPENZI YA DHATI, MIMI NI KIGOLI NA SIJAZAA "...BEUTY...USILALAMIKE UMEKOSA SASA...
Posted by Unknown
Posted on Thursday, October 10, 2013
Mimi
ni mwanamke mjasiliamali mwenye umri wa miaka 25.Ni mzaliwa wa
Sumbawanga ila makazi yangu kwa sasa ni Dar.Sina mtoto na
sijaolewa.
Natafuta mwanaume mwenye mapenzi ya dhati ili awe mume wangu baadae.Mimi sichagui dini wala kabila, ila sipendi mwanaume mgomvi na malaya maana siku hizi kuna magonjwa mengi.
Mwenye nia ya dhati tuwasiliane kwa email yangu ili tupeane namba za simu.
Email:agnessmd2@yahoo.com

MAUAJI YA VIKONGE KANDA YA ZIWA:CHINJA CHINJA WAUA KIKONGWE KWA MAPANGA...PATA HABARI KAMILI...
Posted by Unknown
Posted on Wednesday, October 09, 2013
Mauaji ya kikatili yanayodaiwa kufanywa na Kikundi cha Chinjachinja dhidi ya vikongwe, yamezidi kuutikisa Mkoa wa Geita baada ya kikongwe mwingine, kuuawa kwa kukatwa kwa mapanga akiwa nyumbani kwake.
Marehemu huyo ametajwa kuwa ni, Maua Ikoti(60) mkazi wa Kasang'hwa, wilayani Geita .
Mauaji hayo yamekuja huku takwimu zikionyesha kuwa vikongwe watatu, wameuawa na kikundi hicho katika kipindi cha wiki nne zilizopita.
Baadhi ya watu wanahusisha maujai hayo na imani za kishirikina.
Tukio la mauaji hayo lilitokea saa 6 usiku wa kuamkia juzi baada ya wauaji kuvamia familia hiyo na kisha kuingia ndani ya chumba alimokuwa amekala kikongwe huyo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kasang'hwa, Maganiko Ndiomali, alisema wauaji walimkata kwa mapanga kikongwe huyo kichwani,mikono na kwenye matiti.
Alisema pamoja na mayowe yaliyopigwa na watoto wa marehemu ili kuomba msaada, juhudi za wananchi kuwasaka wauaji hazikuzaa matunda.
Kuna madai kuwa kikundi kinachohusishwa na mauaji hayo kimekuwa kikodiwa na baadhi ya watu ili kulipiza kisasi baada ya kufiwa na ndugu zao wakiamini kwamba wamerogwa.
Kikundi hicho kinadaiwa kuhusika na mauaji ya kikatili dhidi ya Mondesta Nchambi (53) mkazi wa kitongoji cha Isabilo wilayani Chato kwa kumchinja mithili ya kuku.
Kamanda wa polisi mkoani Geita,Leonard Paulo alithibitisha kuwepo kwa matukio hayo lakini alisema hadi sasa hakuna mtu au watu waliokamatwa wakihusishwa na mauaji hayo.
Source-Mwananchi
MAKUBWA: WANAFUNZI WA NGUVUMALI JIJINI TANGA WAFANYA MAPENZI CHOONI NA MADARASANI...
Posted by Unknown
Posted on Wednesday, October 09, 2013
SHULE ya
Sekondari Nguvumali wilayani Tanga, inadaiwa kukumbwa na pepo la ngono
baada ya wanafunzi wake kubainika wakifanya ngono hovyo chooni, madarasani na
njiani wakati wa kwenda na kurudi kwenye makazi yao.
Hali hiyo inadaiwa kusababishwa na kushuka kwa kiwango cha elimu shuleni hapo.
Tatizo hilo liliwekwa hadharani jana na Diwani wa Kata ya Nguvumali, Mustafa Seleboss na Mwenyekiti wa Nguvumali Agness Milambo, kwenye bonanza la kampeni za uzinduzi wa kupinga ukatili mashuleni lililoandaliwa na asasi ya kiraia ya Tree of Hope ya jijini Tanga.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao wa Kata ya Nguvumali, walisema asilimia 80 ya wanafunzi wa Sekondari ya Nguvumali wanafanya mapenzi hovyo hata darasani, vyooni na vichakani wakati wakienda au kurudi nyumbani.
Baadhi ya wanafunzi shuleni hapo, Peter Chambai, Hassan Saidy na Teresia John, wamekiri kufanyika kwa vitendo hivyo viovu, ambavyo wameviita ni ukatili na unyanyasaji wa kisaikolojia dhidi ya wanafunzi wasiopenda mchezo huo mchafu.
Wanafunzi hao walisema washiriki wa vitendo hivyo ni wanafunzi kwa wanafunzi au walimu kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tree of Hope, Fortunata Manyeresa, ameahidi kuingia mtaa kwa mtaa kuwasaka wanafunzi wanaojihusisha na vitendo vya ngono wakiwa na umri mdogo ili wanaowarubuni wachukuliwe hatua.