Home »
AJABU
,
MATUKIO
» MAKUBWA: MWANAMKE AJIMALIZA KWA KUTUMIA MTANDAIO WAKE MWENYEWE...
Posted by Unknown
Posted on Monday, November 11, 2013
|
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema |
MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Maria
Evansi (42) mkazi wa Kijiji cha Kaswira, Nanjara Kibaoni, Tarafa ya
Tarakea wilayani Rombo amekutwa akiwa amefariki dunia baada ya
kujinyonga kwa kutumia mtandio chumbani kwake.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Rombo, OCD, Ralph Meela, amesema tukio
hilo limetokea jana majira ya saa nne asubuhi. Shuhuda wa tukio hilo
ambaye pia ni mtoto wa marehemu, Thea Evans aliuambia mtandao huu kuwa
asubuhi aliondoka nyumbani akamwacha mama yake (marehemu) akiwa mzima
lakini ghafla alishangaa aliporudi alimkuta akiwa ananing’inia juu ya
paa ya nyumba yake akiwa tayari amekwisha fariki.
Hata hivyo, chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika kwani marehemu
hakuacha ujumbe wowote, lakini inasemekana kuwa marehemu alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa akili kwa muda mrefu. Aidha habari kutoka
eneo la tukio zinaeleza kuwa marehemu alishawahi kujaribi kujinyonga kwa
zaidi ya mara nne kwa vipindi tofauti.