muhtasari

Latest Article Get our latest posts by subscribing this site

LULU NJE NJE KUWA MKEO...KAMA UKO TAYARI NI MAHARI YA SH.800,000 OMBI LAKO LIKUBALIKE...Y LAKI NANE...?


Imevuja kuwa mwanaume atakayetaka kumuoa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ atalazimika kutoa si chini ya shilingi laki nane (800,000) kama mahari ili kumuoa mwigizaji huyo.
 
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wanaume wengi wamekuwa wakimendea kufunga ndoa na Lulu lakini wakashindwa njia za kumpata.
 
Ilidaiwa kuwa kikwazo kikubwa wanachokutana nacho ni namna ya kumfikia na kigezo cha dini kwa sababu Lulu hataki kuolewa na muislam kwani hayupo tayari kubadili dini.
 
Akizungumza  katika mahojiano maalum, mapema wiki hii, mama wa Lulu, Lucresia Karugila alisema kwa upande wake yupo tayari kupokea mahari yoyote ilimradi mwanaye awe ameridhiana na mwanaume husika.
 
“Unajua Lulu ameshakua, mambo ya kumwingilia mtoto kwenye vitu binafsi ni ya kizamani. 

“Siwezi kupanga mahari, sijui laki nane au laki ngapi. Kiasi chochote ni sawa cha msingi mwanangu awe amekubaliana na huyo mwanaume.

“Hajaniambia kama kuna mtu anataka kuleta mahari,” alisema mama Lulu.

Kwa upande wake Lulu alisema: “Kwa sasa sina wazo la kuolewa ila naweza kuamka kesho nikabadili uamuzi.” 

 
Alipoulizwa kama ni kweli atatakiwa kulipiwa mahari ya laki nane alisita kidogo.
 
Kuhusu kigezo cha dini staa huyo alikiri kuwa kati ya vitu anavyozingatia ni hicho kwani hataki mwanaume wa kumbadilisha dini na mahari yake itategemea na mtoaji

KWA NINI LAKI 8?
Uchunguzi uliofanywakwa wanandoa wengi waliofunga pingu za maisha hivi karibuni ulibaini kwamba wengi walilipa mahari ya kati ya shilingi laki sita na milioni moja na nusu huku wastani ukiwa ni shilingi laki nane

Credit: >>Global publisher.

OOH MASKINI ...BABU SRYA NA PAPII KOCHA WARUDISHWA TENA KIFUNGO CHA MAISHA...JAMANIIII...



Mwanamziki mkongwe nchini Nguza Viking aka Babu Seya na mwanaye Papii Kocha, wataendelea na kifungo cha maisha jela baada ya mahakama ya rufani nchini kuitupilia mbali rufaa yao iliyosikilizwa leo

Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar ambapo wamekuwa wakikata rufaa mara kwa mara lakini wakagonga mwamba






LULU:" MIMI SIJACHUMBIWA KUOLEWA KUPO TU...TENA MIMI MDOGO"...

 
Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha fununu zilizoandikwa kwenye gazeti la udaku liitwalo ‘Filamu’ kwamba amechumbiwa na muda mchache ataolewa.
 
Akizunguza jana  kwennye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muigizaji huyo wa Foolish Age, alisema hajachumbiwa na mtu yeyote ila ni magazeti ya udaku tu ndio yamekuwa yakiandika kile yanachojisikia.
 
“Mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote aliyenichumbia na kama itatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua, na ni mimi mwenyewe ndiye nitakaesema,” alisema mrembo huyo.
 
“Lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari kutoka kwenye chanzo gani, by the way kwaajili kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu anayejisikia kuandika anaandika ,anaamka anaandika, anaamka anandika. 
 "Kwa hiyo leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, kwa hiyo inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo, kwamba ‘leo Lulu tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe’, I don’t know.
 
“Kuchumbiwa, kuolewa,kuwa mke ni vitu ambavyo tumeumbiwa binadamu, vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa.” Lulu

Ney Lee kufanya listening party ya albam yake jijini Mbeya Nov 17...




Hitmaker wa ‘Umekwenda’ na ‘Nipe Muda’ NEY LEE anatarajia kufanya Listening party ya albam yake ambayo mpaka sasa hajaipa jina, November 17 mwaka huu akianzia nyumbani kwao, Mbeya.
 
Kwenye party hiyo, Super Nyota huyo atasindikizwa na Juma Nature. Akiongea na kipengele cha ‘Chumba Cha Sindano’ kupitia kipindi cha Kali za ‘Bomba cha Kituo’ ya Bomba FM, Mbeya Ney Lee alisema jina la albam hiyo itakuwa ni surprise kwenye uzinduzi huo.
 
“Albam yangu mpaka sasa hivi sijajua itaiitwaje, lakini tayari albam yangu ipo inakuja naanza na Mbeya tarehe 17 nitakuwa Mbeya lakini siwezi kusema ni wapi kwa sababu bado ni mapema na vitu vyote tayari vimeshapangwa lakisi nafikiri soon nitawajulisha wote itakuwa sehemu gani,” alisema.
 
“Nitasindikizwa na JUMA NATURE kwa hiyo nikitu ambacho sasa hivi nipo katika mchakato wa kukifanya na ni kitu serious kabisa. 

"Nita-launch albam yangu mwezi wa 12 kwa hiyo watu watasikiliza nyimbo, na watu wataweza kupiga picha na mimi, kuongea na mimi, kuniuliza maswali mengi coz itakuwa friendly show kwa hiyo watu wengi waje waone wasikie kabla ya kununua kile watakachokinunua wawe wameshakisikia before,” aliongeza.
 
“Kwahiyo nimeanza na Mbeya peke yao ambao wataweza kusikia nyimbo zangu kabla ya kununua albam(kwa msisitizo) ila sehemu nyingine nitauza kawaida tu, sitotaja jina mpaka siku ya show yenyewe.”
 
Kwenye albam hiyo yenye nyimbo nane, muimbaji huyo amewashirikisha wasanii kama Linex, Kala Jeremiah na Ally Nipishe.

NI FURAHA NA NDEREMO KWA BABU SEYA NA PAPII KOCHA...WAKILI WAO ASEMA KAZI IMEKWISHA...



MABERE Nyaucho Marando, wakili wa mwanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ amesema amemaliza kazi ya kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kuwanajisi watoto 12 waliokuwa wakisoma Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na gazeti la  Uwazi juzi, Marando alisema kazi aliyokusudia kuifanya ameimaliza, sasa anasubiri

"WEMA AKAMATWE HARAKA"...KAULI YATOLEWA NA MAHAKAMA...


Mahakama ya mwanzo Kawe jijini dar es salaam imetoa hati ya kumkamata miss tanzania 2006 Wema Sepetu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni dharau ya wito wa mahakama hiyo. 
 
Chanzo cha ndani kilichoomba kuhifadhiwa ya jina kimempasha mwandishi wetu kuwa hati hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya wema kushindwa kuhudhuria kesi yake iliyopo mahakamani hapo na bila kutolewa udhuru wowote. 

Aidha imeelezwa kwamba mahakama hiyo pia imetilia mashaka udhuru uliotolewa septemba 30 kwamba wema ni mgonjwa baada ya kuvuja kwa picha katika mitandao zikimuonyesha Wema akila bata  Hong Kong China na mpenzi wake wa zamani mwanamuziki Diamond. 

Wema alitolewa udhuru huo na kijana aliefahamika kwa jina la Martini .
 Kesi inayomkabili wema katika mahakama hiyo ni ya kumtukana matusi ya nguoni pamoja na kumpiga meneja wa hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe beach jijini Dar es salaam bwana Godluck kayumbu. 

Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi wetu alimtafuta mlalamikaji wa kesi hiyo bwana Kayumbu na kumuuliza kuhusu hati iliyotolewa na mahakama ambapo alithibitisha kuwepo kwa jambo hilo. 

Bwana Kayumbu alisema kuwa amepewa hati  maalum ya kumkamata wema octoba 30 mwaka huu ambayo kesi hiyo ilitajwa tena mahakamani hapo.
Alisema kuwa Wema Sepetu anaweza kukamatwa muda wowote kuanzia sasa kwani octoba 30 mwaka huu kesi hiyo ilitajwa tena mahakama ya Kawe chini ya mheshimiwa hakimu Ikanda lakini wema hakutokea na hakuna mtu yeyote aliyekuja kwaajili ya kumtolea udhuru.
Kayumbu alibainisha kuwa mshtakiwa wake wema sepetu hakuja mahakamani mara mbili mfululizo kuanzia septemba 30 2013 na kudaiwa kuwa anaumwa lakini picha zake katika mitandao zilimuonyesha  akitanua hong kong china na mara ya pili kesi hiyo ilitajwa octoba 30 2013 ambapo hakutokea mtu yeyote anayemuhusu wema katika mahakama hiyo. 

"Kesi ilikuwa ya kwanza kutajwa lakini nilikuwa peke yangu sasa nikaamuliwa mimi nipewe hati maalum ya kumkamata wema ambapo nilipewa na nimeshaikabidhi kituo cha polisi cha kawe kwa utekelezaji maana naona muda unazidi kwenda na kesi haiishi," alisema kayumbu.
Mwandishi  wetu alipomtaarifu bwana kayumbu kuwa octoba 30 Wema Sepetu alikuwa kwenye msiba baada ya kufiwa na  baba yake mzazi mzee Isaac Sepetu na kwamba siku hiyo alikuwa safarini kwenda zanzibar kwa ajili ya mazishi ya mzazi wake huyo, bwana kayumbu alisemaa kuwa suala hilo halimuhusu kwani hata yeye amefiwa na wazazi wake. 
"Kama kafiwa hata mimi nimefiwa na baba na mama yangu pia, kinachotakiwa ni kutii sheria za nchi ikiwemo mahakama ,kama alifiwa kwanini asitoe udhuru? sina mazungumzo tena kinachotakiwa ni sheria ichukue mkondo wake, popote atakapopatikana wema ni lazima akamatwe," alisema Godluck. 
Wema hakupatikana kwenye simu ili kuzungumzia jambo hilo.

-Gazeti  la  Kiu  toleo  la  leo.

MZEE MAJUTO ATANGAZA NIA MWAKA 2015... NI UBUNGE KWA TIKETI YA CCM...



Kwa  mujibu  wa  mtandao wa Bongomovies, msanii  mkongwe wa  vichekesho hapa  nchini, Amri Athumani 'King Majuto' ametangaza kugombea ubunge katika  jimbo  la  Tanga  Mjini mwaka  2015


Majuto  mwenye umri  zaidi ya miaka 60 ametangaza nia yake hiyo alipohojiwa na Clouds  na amedai  kwamba atagombea kupitia CCM.

Juhudi  za  kumtafuta  mzee Majuto ili aweze kututhibitishia kama habari hizi ni za kweli au la na kama ni kweli ana mipango gani na jimbo hilo la Tanga mjini  zinafanyika...

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger