Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha
fununu zilizoandikwa kwenye gazeti la udaku liitwalo ‘Filamu’ kwamba
amechumbiwa na muda mchache ataolewa.
Akizunguza jana kwennye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muigizaji huyo
wa Foolish Age, alisema hajachumbiwa na mtu yeyote ila ni magazeti ya
udaku tu ndio yamekuwa yakiandika kile yanachojisikia.
“Mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote aliyenichumbia na kama
itatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua, na ni mimi mwenyewe ndiye
nitakaesema,” alisema mrembo huyo.
“Lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari kutoka kwenye chanzo
gani, by the way kwaajili kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu
anayejisikia kuandika anaandika ,anaamka anaandika, anaamka anandika.
"Kwa hiyo leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, kwa hiyo
inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo, kwamba ‘leo Lulu
tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe’, I don’t know.
“Kuchumbiwa, kuolewa,kuwa mke ni vitu ambavyo tumeumbiwa binadamu,
vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa.” Lulu