muhtasari

Home » » BARCELONA WAIKATAA OFA YA MAN-U KWA FABREGAS....!!!

BARCELONA WAIKATAA OFA YA MAN-U KWA FABREGAS....!!!

MANCHESTER United inaendelea kukumbana na hali ngumu katika kuwania saini ya Cesc Fabregas baada ya ofa yao ya pili ya pauni milioni 31 nayo kukataliwa na Barcelona.



Na sasa United inajipanga kwenda na ofa ya tatu ya pauni miloni 35 ili kumnyakua kiuongo huyo wa kimataifa wa Hispania.



Lakini mchezaji mwenzake Fabregas katika Barcelona, Gerard Pique ameonya: “United wanapoteza muda wao.



“Imemchukua muda mrefu Cesc kutimiza ndoto yake ya kurejea nyumbani na hatapenda kuipoteza tena. Hapa ni nyumbani mahala ambako familia yake ipo na anacheza na marafiki zake wa karibu.



Ametueleza kuwa yuko na furaha na hana mpango wa kuondoka Barcelona.



Ofa ya kwanza ya United ya pauni milioni 26 ilikataliwa na Barca wiki iliyopita.



Na majibu yalikuwa hayo hayo pale Mtendaji mkuu Ed Woodward alipopeleka ofa ya pili ya pauni milioni 31.



Sasa ni juu ya bodi ya Manchester United kuamua kama kuna haja ya kurudi kwa mara ya tatu.

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger