Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao itaonyeshwa TV kupitia kituo cha Televison cha Azam TV baada ya kamati ya ligi kwa niaba ya vilabu kuingia mkataba wa mabilioni na kampuni ya Azam Media ili kurusha matangazo ya mechi hizo za Ligi kuu kuanzia msimu ujao.
Kwa mujibu wa mkataba huo vilabu vyote vinavyoshiriki kwenye ligi hiyo vitapokea mgawo sawa wa mapato ya uuzwaji wa haki za matangazo ya Television bila ukubwa wala udogo wa klabu husika. Yanga tayari wameshapinga suala hilo la kulipwa sawa na vilabu vingine - JE Wewe kama Mdau wa soka/michezo kwa ujumla una maoni gani kuhusu suala? TUJADILI
source:shaffih blog.