KOCHA WA SIMBA MFARANSA PATRICK LEIWIG KURUDI BONGO KUFUNDISHA SOKA

Kwa mujibu
wa taarifa za kuaminika kutoka chanzo cha habari kilicho karibu na
African Lyon ni kwamba klabu hiyo kwa sasa ipo kwenye mazungumzo mazito
na kocha huyo aliyebobea katika kukuza vipaji vya wachezaji makinda.
"African
Lyon pamoja na kushuka daraja lakini ni timu ambayo inafanya mambo yake
kwa kuangalia mbele zaidi. Sasa wameamua kuwekeza zaidi kwenye timu zao
za vijana na ndio maana wanaamua kumchukua kocha ambaye ana uzoefu
mkubwa wa kukuza vipaji vya wachezaji makinda.
"Mpaka
sasa mazungumzo yanaendelea vizuri na siku chache zijazo tutegemee
kumuona Leiwig akitua Bongo kuja kuiongoza African Lyon," kilikaririwa
chanzo hicho cha habari.
chanzo:shaffih blog.