Kwa ufupi
- Baada ya mshtakiwa huyo kulalamika hivyo, Hakimu Katemana aliutaka upande wa mashtaka uwasilishe hati ya kuzuia dhamana ambayo hata hivyo, hawakuwa nayo licha ya kuwaongezea saa mbili kuandaa.
Mwenendo wa Mashtaka. Kutokana na uamuzi huo wa DPP, Hakimu Lema alimfutia mashtaka Mulundi na kumwachia huru.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye, alikamatwa na kufunguliwa kesi nyingine ya kutoa taarifa za uongo kwa Jeshi la Polisi.
Katika kesi hiyo mpya inayosikilizwa na Hakimu
Mkazi Aloyce Katemana, Wakili wa Serikali Mwandamizi Tumaini Kweka,
alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Julai, 2012, katika Kituo
cha Polisi Oysterbay.
Wakili Kweka alidai kuwa siku hiyo mshtakiwa akiwa
kituoni hapo alitoa taarifa za uongo kwa maofisa wa polisi kuwa yeye na
wenzake ndiyo waliokodiwa ili kumteka na kumdhuru Dk Ulimboka wakati
akijua kuwa si kweli.
Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo.
Wakili Kweka alisema upelelezi wa kesi hiyo
umeshakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa ili waweze kuandaa
maelezo ya awali ya kesi hiyo. Pia aliweka pingamizi la dhamana dhidi ya
mshtakiwa akidai hana makazi ya kudumu kwa kuwa si raia pia kwa ajili
ya usalama wake kulingana na mazingira ya tukio hilo.
Kauli hiyo ya Wakili Kweka ilimfanya mshtakiwa
huyo alipuke na kudai kuwa wanamfungulia kesi za uongo ambazo hahusiki
na kudai kwamba wamepanga kumpoteza.
“Mheshimiwa Hakimu, naomba unisamehe, kwa kile
nitakachokifanya, kwani nikirudi mahabusu mimi itaniumiza,” alidai
mshtakiwa huyo na kusisitiza kuwa hahusiki na kwamba bado ni kijana
mdogo.
Baada ya mshtakiwa huyo kulalamika hivyo, Hakimu
Katemana aliutaka upande wa mashtaka uwasilishe hati ya kuzuia dhamana
ambayo hata hivyo, hawakuwa nayo licha ya kuwaongezea saa mbili kuandaa.
Baada ya kushindwa, Hakimu Katemana alimpa
mshtakiwa masharti ya dhamana, ambayo hata hivyo, naye hakuweza
kuyatekeleza hivyo kurudishwa mahabusu, hadi Agosti 20, mwaka huu kesi
hiyo itakapotajwa.
Masharti hayo ya dhamana yalikuwa ni kuwa na
wadhamini wawili, mmoja akitoka katika taasisi inayofahamika, ambao wote
na yeye, watasaini hati ya Sh5 milioni kila mmoja na kuwasilisha
mahakamani hati zake za kusafiria.
Mulundi alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza
Julai 14, 2012 na kusomewa mashtaka mawili ya kumteka na kutaka kumuua
Dk Ulimboka.
chanzo:mwananchi
chanzo:mwananchi