Home »
MICHEZO
» ARSENAL NDIO MABINGWA WA SERENGETI FIESTA SOKA BONANZA NDANI YA KIGOMA ...
Posted by Unknown
Posted on Saturday, August 17, 2013
 |
MABINGWA WA SERENGETI FIESTA SOKA BONANZA |
 |
Nahodha
wa timu ya mashabiki wa Arsenal mkoani Kigoma Samweli Balina akipokea
kombe la ushindi na kitita cha fedha taslimu laki tatu kutoka kwa
Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba baada ya
kuibuka washindi katika bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza
lililofanyika siku ya ijumaa jioni katika uwanja wa Kawawa uliopo
Ujiji, anayeshuhudia kulia ni meneja wa biashara wa kanda ya ziwa
kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Octavian Migire, na Katibu wa
Chama cha soka mkoani Kigoma Bw. Mrisho Bukuku, Bonanza hilo
limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya
Serengeti Premium Lager. Timu za mashabiki zilizoshiriki bonanza hilo ni
Chelsea, Liverpool, Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, AC Milan. |
 |
Nahodha
wa timu ya mashabiki wa Manchester United mkoani Kigoma akipokea kombe
la ushindi wa pili na kitita cha fedha taslimu laki mbili kutoka kwa
meneja wa biashara kanda ya ziwa kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Bw.
Octavian Migire anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Media
Group Bw. Ruge Mutahaba baada ya kuibuka washindi wa pili katika bonanza
la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililofanyika siku ya ijumaa jioni
katika uwanja wa Kawawa uliopo Ujiji, , na Katibu wa Chama cha soka
mkoani Kigoma Bw. Mrisho Bukuku (mwenye Kaunda suti), Bonanza hilo
limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya
Serengeti Premium Lager. Timu za mashabiki zilizoshiriki bonanza hilo ni
Chelsea, Liverpool, Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, AC Milan. |