muhtasari

Home » , » BREAK NEWS:" KAMANDA WA POLISI MKOANI MOROGORO AMEKANUSHA TAARIFA ZA KUPIGWA RISASI KWA SHEHK PONDA,** NA SASA PONDA ANATAFUTWA NA POLISI...

BREAK NEWS:" KAMANDA WA POLISI MKOANI MOROGORO AMEKANUSHA TAARIFA ZA KUPIGWA RISASI KWA SHEHK PONDA,** NA SASA PONDA ANATAFUTWA NA POLISI...



Taarifa  toka  Morogoro  zinaarifu  kwamba  Sheikh Ponda  amepigwa  risasi  na  polisi  baada  ya  wafuasi wake  kuandamana.....

Taarifa  hizo  zinaeleza  kwamba  Sheikh  Ponda   alikuwa  akiendesha  mhadhara mkoani  Morogoro.Baada  ya  mhadhara  huo, wananchi  walianza  kuandamana  kuelekea  barabarani  ambapo  polisi  walijitokeza  kukabiliana  nao....

Ponda  anadaiwa  kujeruhiwa  wakati  wa  makabiliano hayo  na  haijulikani hali yake  kwa  sasa..
 
Hata  hivyo , kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa  Morogoro,  Faustine Shilogile, amekanusha  madai  hayo  ya  kupigwa  risasi   na  kueleza  kuwa  hali  ni  shwari  mkoani  Morogoro    kwa  sasa  baada  ya  machafuko  ya  muda  mfupi  mida  ya  jioni..

Akizungumzia  kuhusu  Ponda, Shilogile  amesema  kuwa  yeye  hajui hali yake maana polisi walizuia gari lake  ili wamkamate  kwa  tuhuma  za  uchochezi  zinazomkabili, lakini wananchi wakaanza kuwashambulia polisi   na  wakafanikiwa  kumtorosha..

Baada  ya  shambulio hilo, Polisi  walilazimika  kurusha risasi hewani kuwatawanya wananchi . 

Shilogile anatoa  wito  kwa  mtu  yeyote  anayejua  alipo  Ponda awaarifu  polisi  mapema
.

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger