imeidhinisha ujenzi wa nyumba mpya zaidi ya 1,000 katika makaazi ya Wayahudi kwenye maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa na Israel.
Tangazo hilo limetolewa siku tatu kabla ya mazungumzo ya amani baina ya Israel na Wapalestina kuanza tena mjini Jerusalem.
Waziri wa Makaazi wa Israel ametoa idhini ya mwisho kujenga karibu fleti 1,200 katika maeneo yenye makaazi ya Wayahudi, siku tatu tu kabla ya mazungumzo ya amani kati ya Israeli na Palestinian kuanza tena.
Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, alishikilia kwa muda mrefu kwamba hatarejea kwenye mazungumzo bila ya Israel kusitisha kujenga makaazi mepya kwenye maeneo inayoyakalia.
Lakini hatimaye alikubali kushiriki katika mzungumzo baada ya Israel kusema kuwa itawaachilia huru wafungwa wengi wa Kipalestina.
Makaazi ya Wayahudi katika Ufukwe wa Magharibi ndio swala kubwa linalokwamisha mazungumzo.
Makaazi hayo yanaonekana kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa, ingawa Israel inapinga hilo.
-BBC