Chama cha rais aliyetolewa madarakani, Mohammed Morsi, hakikubali juhudi za kupatanisha zinazofanywa na mmoja kati ya viongozi wakubwa wa kidini nchini Misri.
Alisema imamu huyo alipanga njama dhidi ya rais, na aliunga mkono jeshi kumpindua Morsi.
Mohammed Soudan aliongeza kusema kuwa haikuelekea chama chake kuombwa kuzungumza wakati viongozi wake wako jela au wanakabili mashtaka.
Chama hicho ni tawi la siasa la Muslim Brotherhood.
Bwana Soudan piya alionya kuwa maandamano ya wafuasi wa Bwana Morsi yataendelea na kwamba watu wako tayari kufa.
-BBC