Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa Yanga Nurdin Bakari anatarajia kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea timu mpya kwenye Ligi Kuu ya Rhino Rangers ya Tabora.
Kiraka huyo aliyeachwa na Yanga, baada ya kumaliza
mkataba wake Juni mwaka huu na kutupiwa virago, alilithibitishia gazeti
hili jana.
“Niko Tabora kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho kabla ya kusaini mkataba wa kuichezea Rhino katika msimu ujao wa ligi.”
“Kila kitu kinakwenda vizuri. Nafikiri muda siyo
mrefu mambo yatakuwa sawa na kusaini mkataba huo.” alisema Nurdin
aliyekicheza kikosi cha kwanza cha Yanga na Taifa Stars kwa zaidi ya
miaka sita ya mafanikio.
Meneja wa Rhino Rangers, Paul Maganga
alilithibitisha jana kuwa timu hiyo inahitaji huduma ya Nurdin kwa ajili
ya msimu ujao wa ligi:
“Ni kweli, tupo na Nurdin (Bakari) hapa Tabora kwa
ajili ya kufanya naye mazungumzo ya mwisho kusaini mkataba wa kuichezea
timu yetu ya Rhino,”