muhtasari

Home » » SAKATA LA AZAM TV VS YANGA: SERIKALI YAAMUA YANGA NA KAMATI YA LIGI KUPITIA UPYA MKATABA - AZAM MEDIA NA YANGA KUFANYA MKUTANO WA KUJADILI MASLAHI YA WANA JANGWANI

SAKATA LA AZAM TV VS YANGA: SERIKALI YAAMUA YANGA NA KAMATI YA LIGI KUPITIA UPYA MKATABA - AZAM MEDIA NA YANGA KUFANYA MKUTANO WA KUJADILI MASLAHI YA WANA JANGWANI


Hatimaye mkutano ulioitishwa na serikali kupitia wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kusuluhisha mgogoro wa mkataba wa mauzo ya haki za matangazo ya Television uliowashirikisha kamati ya ligi kuu ya soka Tanzania bara, klabu ya Yanga na Azam Media umemalizika hivi punde huku maamuzi kadhaa yakifikiwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha mtandao huu, klabu ya Yanga ni kama imeibuka kidedea kwenye madai yake ya kupinga utaratibu mzima wa mkataba huo baina ya kamati ya ligi na Azam Media. 

Hii inakuja baada maamuzi ya mkutano huo kuamuru kwamba vipengele vya mkataba huo kupitiwa upya na klabu ya Yanga na Kamati ya Ligi na vile ambavyo vitaonekana kuwa na matatizo virekebishwe. 

Pia imeamuliwa kwamba Yanga SC itakaa kikao na Azam Media kuzungumzia mambo mbalimbali ambayo Yanga imeonekana kuwa na shaka nayo kuhusu Azam pamoja na maslahi ya Yanga kupitia dili hilo la ununuaji wa haki za matangazo ya TV ya mechi za ligi uliofanywa na Azam Media. 

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger