Sanamu za mawaziri wakuu wa
zamani wa Uingereza katika bunge la nchi zitatengwa ili kuzuwia wale
wabunge wanaogusa miguu ya sanamu hizo, wakiamini itawapa bahati.
Msimamizi aliiambia kamati ya bunge kwamba
sanamu za viongozi kama Winston Churchill na Margaret Thatcher
zinaharibika kwa sababu ya itikadi hiyo.
Ilani itawekwa, lakini mwenyekiti wa kamati amesema pengine vitawekwa vizuizi iwapo wabunge hawawezi kutuliza mikono yao.
Ilani itawekwa, lakini mwenyekiti wa kamati amesema pengine vitawekwa vizuizi iwapo wabunge hawawezi kutuliza mikono yao.