Posted by Unknown
Posted on Monday, August 05, 2013
KIJANA mmoja ambaye hajafahamika jina lake anayedaiwa kuwa ni jambazi
amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali eneo la Mbezi kwa
Msuguli jijini Dar es Salaam.
Kijana huyo pamoja na mwenzake wakitumia
pikipiki walikuwa na silaha za moto tayari kwa kwenda kufanya uhalifu
lakini kabla mpango wao haujakamilika polisi waliingilia kati na kuanza
kupambana nao.
Haikuwa kazi rahisi kuweza kumkamata jambazi huyo
kutokana na majibizano ya risasi kati yake na polisi.
Baada ya jambazi
lililokuwa linaendesha pikipiki kuona mwenzake anaelekea kukamatwa
lilitokomea wakati mwenzake akiangukia mikononi mwa wananchi wenye
hasira kali waliomshushia kipondo cha nguvu.