Kwa ufupi
Jaji Mutungu anashika nafasi iliyokuwa inashikiliwa
na John Tendwa. Kabla ya Tendwa nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na
George Liundi.
Rais Jakaya Kikwete amemteua Jaji Francis
Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa kujaza nafasi iliyoachwa na John
Tendwa ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilisema kuwa uteuzi huo ulianza
Agosti 2, 2013.
Kabla ya uteuzi huo, Mutungi ambaye ameshika
nyadhifa mbalimbali katika idara ya Mahakama, alikuwa Jaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
Alikotoka
Historia ya Jaji Mutungi katika utumishi wake
mahakamani ilianza mwaka 1989 alipoanza kazi akiwa hakimu, baadaye
akateuliwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Baadaye aliteuliwa na kushika nafasi za Msajili
Mahakama ya Ardhi; Hakimu Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Msajili Mahakama Kuu Kanda
ya Arusha, Msajili Mahakama ya Rufani na hatimaye Jaji katika Mahakama
Kuu Kanda ya Dodoma.
Kuhusu Tendwa
Tendwa ameachia nafasi hiyo akiwa katika msuguano
wa kisiasa na baadhi ya vyama vya siasa, kikiwamo Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) ambacho hivi karibuni kilitangaza kutokumtambua
wala kushirikiana naye.
Katika utumishi wake huo wa miaka 12 tangu
alipoachiwa nafasi hiyo na Jaji George Liundi, Tendwa amekuwa
akishutumiwa mara kwa mara kwa upendeleo dhidi ya vyama vya upinzani,
madai ambayo amekuwa akiyapuuza. Alipotafutwa tena jana kuzungumzia
madai hayo hakupatikana kwa kuwa alikuwa nje ya nchi.
Mbali na Chadema, Tendwa ambaye amewahi
kukwaruzana na vyama cha CUF na TLP, mara nyingine amekuwa akitoa tishio
la kuvifuta vyama hivyo kwa kile alichodai kuwa vinachochea vurugu.
Hali hiyo ilimjengea uhasama baina ya ofisi yake
na vyama vya upinzani na kuna wakati aliwahi kutajwa adui namba moja wa
vyama vya upinzani na demokrasia.
Mkataba wake
- MWANANCHI
- MWANANCHI