muhtasari

Home » , » VURUGU KUBWA ZAZUKA LEO MWANZA, POLISI WAPAMBANA NA WAFUASI WA CHADEMA...

VURUGU KUBWA ZAZUKA LEO MWANZA, POLISI WAPAMBANA NA WAFUASI WA CHADEMA...

Maandamano ya chama cha CHADEMA yaliyokua yanafanyika huko mwanza yamegeuka vurugu baada ya wandamanaji kuanza kupambana na polisi.
CHADEMA walikuwa wakiandamana katika kushinikiza Meya wa Ilemela Henry Matata aachie ngazi kwani hana sifa zakua meya, baada ya kuvuliwa uanachama na chama hicho.

Katika picha zilizokirushwa kupitia televisheni ya Barmedas Tv ya Mwanza, barabara zimeonekana zikiwa zimefungwa kwa mawe na miti, huku katika maeneo mengine uchafu ukiwa umejazwa barabarani na matairi kuchomwa.

Katika mtaa wa Mission waandamanaji wamefunga barabara kwa uchafu uliokua katika dampo moja kando ya barabara hiyo.

Maandamano hayo yalikuwa yamalizikie viwanja vya Furahisha ambapo viongozi wa CHADEMA walitarajiwa kuhutubia.

Chanzo cha vurugu hizo hakijafahamika, ikizingatiwa CHADEMA walikuwa na kibali cha kufanya maandamano hayo.

Hivi sasa polisi wametanda mitaani katika kudhibiti vurugu hizo na hali inaonekana kutengamaa.

- JamiiF0rums

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger