Vilabu vyote viwili vinajinasibu kwamba vipo katika muda wa mapito baada ya kubadilisha makocha, lakini ushindi wa 4-1 wa City dhidi ya majirani zao ulionyesha utofauti mkubwa uliopo baina ya vikosi vya klabu hizi mbili.
City wana ukamilifu kwenye idara, ubora wa ufundi, na matamanio ya dhati ya kurudisha ubingwa wa Premier League chini ya kocha mwenye ufundi mkubwa hasa kwenye mechi kubwa kama hizi.
MSIMAMO WA PREMIER LEAGUE | |||
TIMU 1. Arsenal 2. Tottenham 3. Man City 4. Chelsea ...................... 5. Liverpool 6. Everton 7. Southampton 8. Man Utd | MECHI 5 5 5 5 ........ 5 5 5 5 | GD 5 4 8 4 ........ 2 2 1 1 | Points 12 12 10 10 ........ 10 9 8 7 |
David Moyes alipewa ratiba ngumu - na hata akalalamika kuhusu ratiba hiyo ngumu - lakini mscotish huyu amepata pointi moja tu katika michezo yote mitatu tuliyocheza na timu kubwa zenye upinzani nasi katika ligi na kikosi chake kimecheza kwa kiwango cha kuridhisha kwenye mchezo mmoja tu wa ligi.
Ukiachana na mchezo wa kufungua ligi dhidi ya Swansea, United tumekuwa tukionekana kukosa ubora wa pamoja kama timu, huku safu yetu ya ulinzi ikiyumba hasa kwa viwango vya wachezaji wetu wenye umri mkubwa kiasi kama Rio Ferdinand na Patrice Evra.
Ujio wa Marouane Fellaini katika siku ya mwisho ya usajili ulikuwa muhimu sana, lakini United bado wana tatizo sana katika safu ya kiungo - hawana uimara wa kuweza kufananisha na safu ya kiungo cha Chelsea, City, Tottenham, na sasa hata Arsenal wanaoringia ujio wa 'The Master of Assists' Mesut Ozil na mkabaji Matheiu Flamini.
Kitu kingine cha kuhuzunisha ni upangaji wa kikosi wa kocha, inaonekana bado anafanya majaribio wakati wapinzani wetu wengine wanaogombea TOP 4 wakiwa wameanza vizuri ligi, pamoja na kwamba wamebadilisha makocha na wengine hata wakiwa wameuza wachezaji mategemeo katika msimu uliopita.
United sasa kwa bahati nzuri tuna mechi ambazo angalau unaweza kuziita nyepesi mpaka pale tutakapokutana na 'The inform Gunners' Arsenal November 10. Lakini angalau hizi mechi na timu ndogo tusifanye makosa au Moyes ajiandae kutuletea aibu ya kukosa ubingwa na kukosa hata kushiriki Champions League msimu unaokuja.