*IGP Mwema awafunda kwa saa tatu ofisini kwake
*Wasitisha maandamano, kuunguruma Jangwani leo
Serikali imesema kauli zilizotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Bw.Freeman Mbowe na Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi(CUF),zinahatarisha amani ya nchi.Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Bi.Sophia Simba,aliyase mahayo Dar es Sa laam jana katika mkutano wake na waandishi wa habari.Alisema viongozi hao walitoa kauli hizo Septemba 21,mwaka huu,katika Viwanja vya Jangwani, Dare s Sa laam na kuongeza kuwa, kauli hizo zinaweza kuleta madhara kwa jamii hasa wanawake,watoto, wazee na walemavu.Aliongeza kuwa,lengo la viongozi hao kupitia muungano wa vyama vya upinzani ni kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete asisaini Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013 ili kuwa sheria kamili.Alisema katika mkutano huo, Prof.Lipumba alisema "Vijana msikubali wakati wa kufanya mazoezi ume fika"na kuhoji mazoezi hayo ya aina gani,yatafanyi ka wapi,kwa lengo gani na kutoa wito kwa wananchi, wasikubali kutumiwa katika mambo yasiyo na tija.Bi.Simba alisema, Bw.Mbowe alisema"Oktoba 10 mwaka huu ni siku maalum ya kitaifa ya Civil Disobedie nce,"na kudai kauli hiyo ni ya hatari yenye kiashiria cha uwepo wa njama mbaya za kushawishi wananchi ili siku hiyo wajichukulie sh eria mkononi kinyume cha katiba,sheria na haki za binadamu."Hii ni kauli hatari, maana yake ni siku maalumu ya kitaifa ya jamii kutotii kuanzia ngazi ya familia.. haya yakitokea itakuwa ni siku angamizi,jamii kutotii ni utovu wa nidhamu ambao husababisha uvunjifu wa sheria na kuhamasisha mazingira ya vurugu," alisema Bi. Simba.Akizungumzia kauli ya Bw.James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Ma geuzi, Bi. Sophia alisema ni yakizalendo na inapaswa kuungwa mkono na kusisitiza kuwa, Mwenyekiti huyo anaonekana ni mtu mwenye kutambua dhama na ya kuilinda familia yake na jamii ya Watanzania kwa ujumla.Katika mkutano huo, Bw. Mbatia alisema"Kuna fursa ya kukaa katika round table(meza ya duara) na kuyazungumza." Alisema kauli za wanasiasa wengine,hazikuwa nzuri kwa maendeleo na ustawi wa kijamii na kiuchumi."Siku hii ya Civil Disobedience, mamalishe na wajasiriamali wengine hawatafanya biashara zao,wat oto hawataenda shule na huduma nyingi za kijamii zitakwama wakati wao wakipanga kutekeleza mipango waliyopanga kwa tarehe hiyo,"alisema.Aliitaka jamii itambue kuwa, amani na usalama ndiyo mtaji namba moja wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia na ustawi wetu kama jamii ya Wa tanzania au familia unahitaji uwepo wa amani,utulivu na usalama .
CHADEMA wajibuAkijibu tuhuma hizo kwa niaba ya Muungano wa vyama vya upinzani,Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho Bw.John Mnyika, alisema muungano huo umeshangazwa na kauli ya Bi.Simba na kudai ametumwa.Akizungumza na waandishi wa habari,Bw.Mnyika alisema maelezo ya Bi.Simba hayana mashiko ambapo vyombo vya Ulinzi na Usalama ndio vinavyopaswa kulisemea suala zima la mkutano wao walioufanya Se ptemba 21,mwaka huu.“Waziri Simba asitake kuwatisha wananchi,mkutano wa Oktoba 10 mwaka huu,utafanyika vizuri iwe Rais Kikwete amesaini ama la... kinachoonekana sasa ni kwamba,Serikali inaanza kujihami wakati vyama na taasisi nyingine za kidini tumesema tutaf anya maandamano ya amani kudai haki yetu.“Kinachofany ikasasaniupotoshaji ambaohatu kubali ani nao ,kwanin iWaziriSimbaawe wak wanzak uuseme a mku tanowetuwenyele ngo lakufanyamazungumz onawa nanchi,” alisema.Aliongeza kuwa, hawapo tayarikukub alivitishonakamaWaziri huyoana tambua vio ngozi wanatakiwa kutii sheria bila shuruti, kwanini neno hilo linatumiwa vibaya na watawala.“Anatumia kauli za viongozi walizozitoa katika mkutano wa Jangwani ili kulinda hoja zake akisema, maandamano yetu ni ya uchochezi jambo ambalo si kweli.“Mkutano huu unakubalika na nchi nyingi zimewahi kufanya hivyo, Waziri Simba angekuwa muungwana angeanza kwa kuwatetea vijana na walemavu,” alisema Bw. Mnyika.
-majira