Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Bw.Zitto Kabwe(CHADEM A),ameandika barua
kwenda kwa Katibu wa Bunge akimkumbusha azimio la Bunge namba 9/2012
kuhusu Watanzania walioficha fedha nje ya nchi.
Katika barua hiyo,Bw.Zitt oalisema Mkutano wa Tisa wa Bunge la 10
uliofanyika mwezi Novemba 2012,kutokana na hoja binafsi ya mbunge,Bunge
lil ipitisha Azimio la Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma
za Watanzania kuficha mabilioni ya fedha za kigeni katika Benki za
Ughaibuni hasa nchini Uswisi.Alisema Bunge liliagiza taarifa ya utekelezaji wa Azimio hilo iwe
imewasilishwa bungeni kwenye Mkutano wa 11(Aprili,2013).Kutokana na
kubadilishwa mfumo wa Bajeti ya Nchi,mkutano huo ulikuwa wa bajeti hivyo
ilitaraji wa taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa azimio
hilo,ingewasilishwa bungeni katika mkutano wa Agosti-Septemba 2013
lakini ilishindikana. " Pamoja na kwamba hoja ikishaamuliwa na Bunge ni hoja ya Bunge si
ya mtoa hoja tena...nikiwa mdau mkubwa kwenye hoja hii, napata mashaka
kwa nini Serikali imeshindwa kuwasilisha taarifa bungeni kwa mujibu wa
Azimio la Bunge. "Kutowasilishwa taarifa hii,kunaleta wasiwasi miongoni mwa wananchi
kuwa hoja husika imetupwa kapuni na Taifa halitapata ukweli kuhusu
utoroshaji wa fedha za kigeni nje na kufichwa katika benki au kununua
mali ughaibuni kama majumba,"alisema.Bw. Zitto aliliomba Bunge liitake Serikali iwa silishe taarifa hiyo
juu ya utekelezaji wa Azimio la Bunge namba 9/2012 kuhusu Watanzania
walioficha mabilioni nje kwenye mkutano wa Bunge uliopangwa kuanza
Oktoba 29, mwaka huu
-majira