Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willibrod Slaa katika ziara yake nchini Marekani iliyoandaliwa na umoja wa vyuo vikubwa nchini humo ya kujifunza mambo mbali mbali, imemfikisha leo katika jimbo la Alabama na kupokelewa na wakuu wa jimbo hilo akiwemo Gavana pamoja na Waziri wa biashara.
Alabama ni moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma sana kiuchumi na kimaendeleo siku za nyuma. Uchumi wake ulitegemea kilimo kwa 90%. Miaka 25 iliyopita, viongozi wake walibuni mikakatati ya kulibadilisha. Leo, Jimbo la Alabama ndio moja ya majimbo yenye viwanda vikubwa vya magari kama Honda, Mercedes Benz, Airbus, Hyundai, Raytheon, Space station, Wallgreens na mengineyo Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa.
Uongozi wa jimbo na Dr. Wakila chakula cha mchana iliyotayarishwa kwa ajili yake
Dr. Slaa akimshukuru mmoja wa askari waliokuwa wakiongoza msafara wake
Kupitia kauli mbiu yake ya “Vision Tanzania” Dr. Slaa alipata kukutana na viongozi wa jimbo hilo ili aweze kujifunza mbinu ambayo ataweza kuwarudishia watanzania ili nao waondokane na umasikini. Licha ya yote, Gavana wa jimbo hilo pamoja na mawaziri wake, wako tayari kushirikiana na Tanzania kwenye mambo ya biashara hasa miundombinu ikiwemo bandari, ujenzi wa madaraja na bandari. Dr. Slaa na mkewe Josephine walipokelewa na Gavana pamoja na mawaziri wake
Dr. Slaa, gavana na mawaziri wake wakiwa katika mjadala wa ushirikiano
Dr. Slaa Akimkabidhi Waziri wa Biashara Sera za Kiuchumi za Chadema
Dr. Slaa kwenye picha ya pamoja na gavana
Kubwa ya yote alichojifunza Dr. Slaa ni kwamba, serikali inaweza kuwa na ufanisi hata ikiwa na baraza dogo. Jimbo la Alabama lina Mawaziri sita tu, huku CCM ikiwapa walipa kodi wa Tanzania mawaziri 70 wasiokuwa na kazi. Wengi wao wakiwa na matumizi makubwa huku wakina mama wakijifungua sakafuni, walimu wakinyimwa haki zao, polisi na wanajeshi wakiishi hali duni na wanafunzi wakisoma chini ya miembe. CCM ni janga kubwa lililowakumba watanzania
Chuo Kikuu Cha Kilimo Auburn
Kadhalika Dr. Slaa ametembelea chuo kikuu cha auburn ambayo ni moja ya vyu vikuu vikubwa zaidi vya utafiti duniani. Auburn Inafanya shuguli zake nchini Kenya, Uganda, Senegal na kwingineko barani Afrika. Nchini Kenya, chuo cha auburn inawasaidia wakulima mbalimbali hasa wafugaji wa samaki na technologia za kisasa inayowawezesha kusafirisha samaki wengi kwenda ulaya Ulaya. Kati ya Kenya na Uganda, utafiti wao umetoa zaidi ya ajira 7000.
Walipoulizwa kwa nini walikwepa Tanzania, hawakuficha ukweli. Walinena kwamba ni vigumu sana kufanya kazi Tanzania. Ufisadi uliwazuia ingawa wangekuja na fedha zao kutoka benki ya dunia na shirika la kimarekani la USAID ambayo inadhamini miradi yao sehemu nyingi barani Afrika ikiwemo Kenya na Uganda. Viongozi wa chuo hicho wako tayari kurudi Tanzania ikiwa mazingira ya kazi yatabadilika hasa kukiwepo na serikali mbadala, ambayo Mh. Slaa amewahakikishia kwamba Chadema hiko tayari kufanya nao kazi.
Viongozi wa Auburn University wako tayari kusaidia vyuo vya Tanzania kama Sokoine kwa kuwafundisha waalimu na pia kubadilishana nao technolojia za kisasa za kilimo. Wako pia tayari kuwafundisha wakulima wa aina zote na hata walaji mbali mbali mbali.
Dr. Slaa akiwasili chuo kikuu cha Kilimo Cha Auburn. Nyuma yake ni walinzi kwenye msafara wake
Dr. Slaa akiwa kwenye mazungumzo na uongozi wa chuo cha kilimo
kushirikiana na vyuo vikuu vya tanzania kwa lengo la kubadilishana
teknolojia na ujuzi ili kuinyanyua kilimo cha tanzania na pia kuongeza
ajira
Dr. Slaa akilakiwa na Dean wa Chuo cha Kilimo pamoja na viongozi wengine wa juu wa chuo hicho