Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Khangi Lugola, akichangia mjadala wa Kamati za tatu za Bunge zinazohusu fedha, bungeni Dodoma juziRais Jakaya Kikwete, ameshauriwa kumng’oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikielezwa sababu kuwa ndiye kikwazo katika utendaji wa Serikali na kwamba akiachwa ataipeleka pabaya Serikali na CCM.
Kikwete pia ameshauriwa kumfukuza kazi Waziri wa
Tamisemi, Hawa Ghasia, kwa kushindwa kukabiliana na matatizo ya
ubadhirifu katika halmashauri nchini.
“Kama (Rais) unaitakia mema nchi na CCM kuchukua
hatua za kuwafukuza kazi Pinda na Waziri Ghasia,” alisema Mbunge wa
Mwibara, Khangi Lugola (CCM), juzi alipochangia taarifa za Kamati za
Bunge kuhusu hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30
mwaka jana.
“Kwa nini Watanzania wafe kwa kunyimwa misaada na
wafadhili kwa sababu ya mtu mmoja tu Pinda, kwa ajili ya Ghasia
ameiendesha Tamisemi kama Saccos ama Vikoba?” alihoji.
“Mchawi wetu ... ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda
amekuwa mpole mno hawajibiki,” alisema Mh. Lugola na kuongeza, “Kuanzia
jana (juzi) Waziri Mkuu anahudhuria mahafali.”
Wakati Lugola akizungumza mawaziri waliokuwepo bungeni ni wanne, manaibu mawaziri wawiliwawili, wakati mawaziri wote 53.
-mwananchi
-mwananchi