muhtasari

Home » , » LEO NDIYO LEO:ZITTO KUFUNGUKA MASHITAKA YAKE 11 ANAYOTUHUMIWA NA CHADEMA,YATAJIBIWA NA MWANASHERIA WAKE MBELE YA WAANDISHI WA HABARI...

LEO NDIYO LEO:ZITTO KUFUNGUKA MASHITAKA YAKE 11 ANAYOTUHUMIWA NA CHADEMA,YATAJIBIWA NA MWANASHERIA WAKE MBELE YA WAANDISHI WA HABARI...


MWANASHERIA wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, Ndugu Albert Msando, atazungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika Hoteli ya Serena leo tarehe 11/12/2013 kuanzia saa nne na nusu asubuhi (saa 4.30 asubuhi)

Dhima ya mkutano huu itakuwa kutoa ufafafunuzi juu  ya mashitaka 11 na majibu yake  ambayo Mhe. Zitto Kabwe  na washitakiwa wenzake walipewa na Kamati Kuu ya CHADEMA. Aidha, katika kikao hiki Ndugu Msando, kwa niaba ya wateja wake, ataeleza hatua ambazo wateja wake wanazichukua ndani ya chama katika kuhakikisha kwamba mgogoro uliopo unakwisha kwa amani na haraka iwezekanavyo bila kuleta athari zaidi kwa chama.

Tunatanguliza shukrani na tunaomba waalikwa wazingatie muda.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe,
Jumanne, 10 Desemba 2013
Dar es Salaam


Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger