Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akimsikiliza Dkt. Mugisha Clement, aliyekuwa akimpa maelezo
kuhusu alivyompokea Mjumbe wa Tume ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi,
aliyelazwa katika Kitengo cha Uangalizi Maalum (ICU) MOI katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipokwenda kumjulia hali, kufuatia
kujeruhiwa na majambazi usiku wa kuamkia jumapili huko nyumbani kwake
maeneo ya Kibamba.