muhtasari

Home » , » KIJANA ACHINJWA KAMA KUKU RUKWA...KISHA WAUAJI WAONDOKA NA KICHWA CHAKE...

KIJANA ACHINJWA KAMA KUKU RUKWA...KISHA WAUAJI WAONDOKA NA KICHWA CHAKE...

 
MATUKIO ya mauaji ya kikatili yameendelea kushamiri mkoani Rukwa, baada ya watu wasiojulikana kumuua kikatili mtu mmoja kwa kumchinja na kutokomea kusikojulikana na kichwa cha mtu huyo.

Baadhi ya askari polisi wakitelemsha maiti ya mtu ambaye ameuawa kwa kukatwa kichwa na watu kutoweka na kichwa chake usiku wa kuamkia jana kwa ajili ya kuhifadhi katika hchumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya mkoa iliyopo mjini Sumbawanga.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, watu hao baada ya kufanya mauaji hayo walikwenda kumtupa kwenye eneo hilo ambapo asubuhi ya kuamkia jana  kiwiliwili chake kilibainika kuwepo hapo bila kichwa kwani waliondoka nacho.
 
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa polisi inaendelea kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger