Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mlemavu Debile James kutoka
katika kijiji cha Bulega wilayani Bukombe Mkoani Geita muda mfupi baada
ya kufungua shule ya msingi Ng’anzo iliyojengwa na kampuni ya madini ya
Nsagali yenye makao yake wilayani humo.Rais Kikwete aliahidi kumpatia
Bajaji Mlemavu huyo ili aweze kumudu shughuli zake za kujitafutia
kipato. Rais Kikwete yupo katika ziara ya siku tano mkoa mpya wa Geita
kukagua na kuzindua shughuli za maendeleo.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria kuzindua Mkoa
mpya wa Geita jana mchana.Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa TAMISEMI
anayeshughulikia elimu Kassim Majaliwa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita
Magalula Said Magalula.
Wazee
wa Mkoa wa Geita wakimvisha Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete vazi la
kijadi wakati wa uzinduzi wa Mkoa Mpya wa Geita Jumamosi mchana.