muhtasari

Home » , , , » WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WASHANGAZWA NA AVAMIZI FEKI WA ALI-SHABAAB ULIOFANYIKA NDANI YA HOTEL YA GOLD CREST…

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WASHANGAZWA NA AVAMIZI FEKI WA ALI-SHABAAB ULIOFANYIKA NDANI YA HOTEL YA GOLD CREST…

Wakazi wa jiji la Mwanza juzi  majira ya saa 4 asubuhi waliwekwa njia panda na kujawa hofu kubwa kufuatia vikosi vya askari kanzu, FFU, askari polisi na zimamoto wakiwa na vifaa sambamba na magari yao walipolivamia jengo la Hotel Gold Crest na kuanza saka saka za kujiweka sawa huku wakiendeleza mapambano na jamaa ambao walijipanga mithili ya wahalifu.

Hali hiyo ilisababisha magari pikipiki kusimama kwa muda huku wananchi wakiingiwa hofu na woga, wengine wakikimbia na baadhi ya wafanyabiashara walifunga maduka yao wakifananisha na lile la Westgate la jijini Nairobi nchini Kenya..
 
Hata hivyo mpaka zoezi hilo linamalizika hakuna mwananchi aliyeweza kubaini kuwa tukio hilo lilikuwa ni la uigizaji, kila mmoja alikuwa akisimulia kivyake sekeseke zima, lakini mapango mzima ulikuwa ni kuvinoa vikosi vya polisi na Zimamoto juu ya kukabiliana na uhalifu kwenye majengo makubwa ya huduma mbalimbali.  



Wateja wa kituo cha mafuta kilichopo karibu na hotel Gold Crest jengo ambalo ndiko zoezi lilikuwa likifanyika pamoja na wateja wa ofisi za PPF, duka la Vodacom Mwanza na Benki ya NMB zilizopo katika jengo hilo walikosa huduma kwa muda huku wengine wakitimka maeneo hayo kwa tahadhari wakidhani ni live.




Watu wakihaha nao polisi wakiweka ulinzi mkali eneo la tukio. 


Harakati zikiendelea eneo la tukio.
Polisi wakiwaweka chini ya ulinzi 'wahalifu bandia' katika zoezi lililozua taharuki kwa kwakazi wa jiji laMwanza.

Popular Post

 
Support : OBAMA | OBAMA | OBAMA
Copyright © 2013. DiraYaLeo - All Rights Reserved
Template Created by Barakaeli Aremu Published by Dira Ya Leo
Proudly powered by Blogger